Home Mchanganyiko UZINDUZI WA KITABU CHA KUVUTIA WATALII ‘A TASTE OF TANZANIA”

UZINDUZI WA KITABU CHA KUVUTIA WATALII ‘A TASTE OF TANZANIA”

0
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Uzinduzi wa Kitabu cha ‘A
TASTE OF TANZANIA”
Dodoma,
5 Februari 2020
Ubalozi
wa Tanzania nchini Uholanzi umeshiriki katika hafla ya uzinduzi wa kitabu kinachoitwa
“A
Taste of Tanzania”
kilichosheheni picha zinazoonesha vivutio vya utalii pamoja na utamaduni wa
Mtanzania. Uzinduzi wa Kitabu hicho chenye kurasa 343 ulifanyika wakati wa ufunguzi
wa maonesho ya picha za utalii uliofanyika The Hague, Uholanzi tarehe 30
Januari 2020.
Maeneo
ya utalii yanayooneshwa kwa kina ndani ya Kitabu hicho ni pamoja na; Mji wa
kimataifa wa Arusha; Mlima Kilimanjaro; Hifadhi za Taifa za Manyara,
Ngorongoro, Serengeti, Tarangire na Ruaha; Mlima Ol Donyo Lengai na Ziwa
Natron. Maeneo mengine ni Olduvai
Gorge; umaarufu wa Ziwa Eyasi na Bonde la Ufa; Utalii wa mkoa wa Iringa;
aina mbalimbali za mapishi pamoja na viungo vyenye ladha nzuri vinavyoleta
upekee katika mapishi hayo.
Katika
hotuba yake ya ufunguzi wa sherehe ya Uzinduzi wa Kitabu na Maonyesho hayo,
Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju aliwashukuru waandaji
wa Kitabu hicho kwa uwasilishaji sahihi kuhusu Tanzania, hali itakayowezesha
watalii kuongezeka zaidi nchini, Balozi Kasyanju alitumia fursa hiyo pia kutoa
wito kwa Waholanzi na Jumuiya ya Kimataifa kuja kuwekeza Tanzania kufuatia
maboresho makubwa yaliyofanyika katika miundombinu na taratibu za uwekezaji.
“A
Taste of Tanzania” ni kitabu kilichoandaliwa na mwandishi Bw. Stephen Walckiers kwa kushirikiana na mpiga
picha maarufu, Bw. Wim Demessemaekers, wote wakazi wa Uholanzi waliowahi pia
kuishi Tanzania. Uzinduzi
rasmi wa kitabu hicho kinachopatikana kwenye mitandao na maduka ya vitabu
nchini unatarajiwa kufanyika nchini Tanzania tarehe 05 Februari 2020.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.
=======================================================================
 
 
Baadhi ya picha zilizotumika kuutangaza utalii wa Tanzania katika kitabu cha “A Taste of Tanzania.” 

 

 

Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju akiteta jambo na mpiga picha aliyeshiriki katika maandalizi ya uandishi na uchapishaji wa kitabu hicho, Bw. Wim Demessemaekers.

 

Mhe. Balozi kasanju akipokea ufafanuzi wa tafsiri za picha mbalimbali kutoka kwa Bw. Wim

 

Balozi wa Yemen nchini Uholanzi, Mhe. Sahar Ghanem akimsalimia na kumpongeza Bw. Wim kwa umahiri wake wa kupiga picha. Mhe. Ghanem
alielezea nia yake ya dhati ya kutembelea
Tanzania.

 

Sehemu ya Wanadiplomasia, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa na wadau wengine walioshiriki kwenye sherehe ya uzinduzi wa Kitabu na ufunguzi wa maonesho ya picha za utalii wa Tanzania.
 
Baadhi ya vyakula vya kitanzania vilivyoandaliwa kwa ajili ya hafla ya uzinduzi wa kitabu na ufunguzi wa maonesho.