Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi kutoka katika taasisi hiyo, Bw. Frank Matua akitoa taarifa fupi kuhusu watoto wanaozaliwa na vichwa vikubwa.
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Mhe. Martha Mpaze akishusha vitu mbalimbali vilivyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo kwa ajili ya kusaidia watoto waliozaliwa na vichwa vikubwa wakiwemo mama zao ambao wanapata matibabu katika Taasisi ya Mifupa (MOI), iliyopo kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili. Ikiwa ni moja ya huduma waliyoifanya katika kuadhimisha Wiki ya Sheria ya mwaka huu.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Ruth Massam (kushoto) akitoa elimu ya sheria kwa wakina mama ambao wenye watoto waliozaliwa na vichwa vikubwa ambao wanapata matibabu katika Taasisi ya Mifupa (MOI), iliyopo kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Ruth Massam (kushoto) akiwakabidhi vitu mbalimbali wauguzi wa Taasisi ya Mifupa (MOI), iliyopo kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili wanaohudumia watoto waliozaliwa na vichwa vikubwa ambao wanapata matibabu hospitalini hapo.