Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (kushoto) akipokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima, katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dodoma, leo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio akizungumza katika kikao cha makabidhiano kati yake na aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima (kulia), katika ukumbi wa mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Makabidhiano hayo yalihudhuriwa na viongozi wa Wizara hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (katikati) akimsikiliza aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima, baada ya makabidhiano ya ofisi yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (katikati) akimsikiliza Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu wa Wizara hiyo, Emmanuel Kayuni, baada ya Katibu MKuu huyo, kukabidhiwa Ofisi na Kaimu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima (wapili kulia) katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio akizungumza katika kikao cha makabidhiano kati yake na aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima (kushoto kwa Katibu Mkuu), katika ukumbi wa mikutano wa Wizara, jijini Dodoma, leo. Makabidhiano hayo yalihudhuriwa na viongozi wa Wizara hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi, Sudi Mwakibasi, wakati Katibu Mkuu alipokuwa anawasili Wizarani, jijini Dodoma, leo, kwa ajili makabidhiano ya ofisi kati yake na aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima (kushoto). Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
……………………………………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu, MOHA, Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio, amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara yake wafanye kazi kwa ushirikiano na wawe wazi ili kuondoa changamoto mbalimbali zilizopo ndani ya Wizara hiyo.
Akizungumza baada ya makabidhiano ya ofisi kati yake na aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima, yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo jijini Dodoma, leo, Katibu Mkuu Kadio amewataka viongozi hao kufanya kazi kwa pamoja na kuwa wazi ili kuiletea Wizara na Serikali kwa ujumla mafanikio chanya.
“Nashukuru kwa kunikaribisha, nimefurahi kuwa nanyi, ila tufanye kazi kwa mashauriano kwa pamoja, ili tuweze kutatua changamoto mbalimbali ambazo kila Wizara wanazo, na pia nasi tunazo, “ alisema Kadio.
Pia Kadio alielekeza kuonana na kila Mkuu wa Idara na Kitengo baada ya makabidhiano hayo, ili kusikiliza majukumu yao, pamoja na kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili na kutafuta njia ya kuzitafua.
“Nataka mje tuzungumza, kila mmoja wenu aje ofisini kwangu tuzungumze, na pia muwe wazi, muwe wakweli ili nijue majukumu yenu, changamoto zenu ili tuweze kusaidiana,” alisema Kadio.
Katibu Mkuu Kadio pia aliwapongeza kwa kazi nzuri ambazo Wizara imekuwa inazifanya kwa kipindi chote na kupitia utendaji huo mzuri kuna maboresho na mafanikio ya mambo mbalimbali ndani ya Wizara.
“Nawapongeza kwa kazi nzuri mnazozifanya licha ya kuwepo kwa changamoto lakini tutapambana nazo, kuna maboresho na mmefanikiwa mambo mengi na bado tuna fursa ya kufanya mazuri zaidi,” alisema Kadio.
Pia Kadio alisema anapenda kila kiongozi kuwa wazi, na kusema yoyote bila woga kwasababu anataka ukweli katika utendaji wake wa kazi.