**************************
NJOMBE
Askari 3 wamefariki dunia papo hapo na wengine 9 kujeruhiwa vibaya baada ya gari ya polisi yenye nambari za usajiri PT 3734 kugonngana na basi la abiria la kampuni ya Sharon lenye nambari za usajiri T349 CXB linalofanya safari zake Njombe -Arusha.
Kamanda wa jeshi la polsi mkoa wa Njombe Hamis Issa akizungumzia tukio hilo anasema ajari imetokea majira ya saa kumi na mbili na robo asubuhi jirani na makao makuu ya jeshi la polisi na kusababisha vifo na majeruhi kwa askari waliokuwemo katika gari la polisi lililokuwa libeba askari 12 wakipelekwa lindoni.
Akifafanua zaidi Kamanda Issa amesema katika majeruhi 9 wawili wamepata majeraha makubwa eneo la kichwa ambapo baada ya kukimbizwa hospitali nane wamepata ahueni huku mmoja ambaye amevunjika shingo akipewa rufaa ya kwenda Muhimbili MOI kwa matibabu zaidi na kutakiwa kusafirishwa kwa ndege.
Kuhusu chanzo cha tatizo kamanda huyo amekanusha tuhuma za basi kufeli breki kama ambavyo inaenezwa na kudai kwamba uchunguzi wa awali umebaini dereva wa basi alikuwa na mwendo wa kasi jambo ambalo lilisababisha kushindwa kukabiliana na ajari hiyo.
Nae mganga mfawidhi wa hospitali ya halmashauri ya mji wa Njombe KIBENA Alto Mtega anakiri kupokea majeruhi 9 na miili 3 na kudai kwamba jitihada kubwa za matibabu zikichukuliwa kwa majeruhi 8 huku mmoja ambaye amevunjika shingo akilazimika kusafirishwa kwa ndege kwenda hospitali ya taifa muhimbili kwa matibabu zaidi
Mustafa Said ambaye ni manusura wa ajari hiyo aliyepatiwa matibabu na kupata ahueni anasema hakuoana chochote kilichotokea zaidi ya kujikuta wagongwa na kurushwa nje ya gari na wengine kuzimia .