Waziri wa Madini Doto Biteko akihutubia wananchi waliohudhuria kwenye mkutano huo kabla ya zoezi la kukabiidhi funguo za ofisi za serikali za vijiji vitatu.
Waziri wa Madini Doto Biteko akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili wilayani Ulanga mkoani Morogoro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mahenge Resources Ltd John De Vries akitoa hotuba yake kabla ya kukabidhi funguo za vijiji vitatu vya Nawenge, Kisewe na Mdindo wilayani Ulanga kwa Waziri wa Madini.
Waziri wa Madini Doto Biteko mara baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye moja ya ofisi ya serikali ya Kijiji cha Kisewe Wilayani Ulanga zilizojengwa na Mahenge Resources Ltd. Kulia kwa waziri ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mahenge Resources Ltd John De Vries na kulia ni Mbunge wa Mahenge Goodluck Mlinga.
********************************
Na Issa Mtuwa – Ulanga
Waziri wa Madini Doto Biteko amesema tangu kuanzishwa kwa soko la madini Ulanga wamenunua madini ya Tsh 396 milioni ndani ya miezi 5 mpaka sasa na kwamba awali kabla ya kuanzishwa kwa soko hilo walikuwa wanauza madini hayo kwa milioni 4 tu kwa miaka 5. “Kwa nini
nisiseme naongea kwa takwimu? alisema Biteko.
Amesema hayo jana tarehe 1/2/2020 wilayani Ulanga wakati wa ghafla ya kukata utepe na kukabidhi ofisi na funguo za serikali za vijiji vitatu vya Nawenge, Kisewe na Mdindo, zilizojengwa na mwekezaji wa Mahenge
Resources Ltd katika hatua zake za awali kabla ya kuanza kuchimba madini ya graphite.
“Madini yamechimbwa muda mrefu sana, lakini madini haya yalikuwa hayaachi alama kwenye jamii zetu, nafurahi kuona Mahenge Resources Ltd wanampango wenye kuweka alama kwa shughuli zao kwa jamii yetu.
Mipango yao iko wazi juu ya maslai ya wananchi, nimemwagiza Mkuu wa wilaya Ngollo Malenya asimamie yale yote yaliyokubaliwa kwa ajili ya utekelezaji”. alisema Biteko.
Akikabidhi funguo za ofisi hizo kwa waziri wa madini, Mkurugenzi Mtendaji wa Mahenge Resources Ltd, John De Vries, wanafurahi kuungana na waziri ili wamkabidhi majengo ya serikali za vijiji vitatu.
“Tupo teyari kwa ajili ya kutekeleza yale yote tuliyokubaliana” alisema Vries.
Kwa upande wake, Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga alimshukuru Waziri wa Madini kwa kufika kwake. Alisema madini ya Ulanga yamechimbwa muda mrefu lakini hayajatupa faida, awamu hii tunaona yameanza kutupa faida.
Mlinga alisema ni bora mtu akumbatie transformer ya umeme anaweza kupona kuliko kuchezea maslai ya watu wake wa Mahenge, kamwe hata kubaliana nae.
Mkuu wa Wilaya hiyo Ngollo Malenya alisema uongozi wa wilaya na timu yake wanafurahi kwa uwepo wa wawekezaji hao, ni imani ya uongozi kuona mchango mkubwa wa kimaendeleo hasa kwenye ulipaji wa kodi ya
Halmashauri yetu na utekelezaji wa maendeo kwa ajili ya wananchi.