Mohamed Salah akishangilia baada ya kuifungia mabao mawili Liverpool dakika za 71 na 90 katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Southampton, mabao mengine yakifungwa na Alex Oxlade-Chamberlain dakika ya 47 na Jordan Henderson dakika ya 60 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield leo. Ushindi huo, unaifanya Liverpool ifikishe pointi 73 katika mchezo wa 25 na kutanua uongozi wake sasa ikiizidi pointi 22 Manchester City inayofuatia kwa pointi zake 51 za mechi 24 PICHA ZAIDI SOMA HAPA