Home Mchanganyiko MASAUNI AHOJIWA TAKUKURU JIJINI DODOMA

MASAUNI AHOJIWA TAKUKURU JIJINI DODOMA

0

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni akitoka katika Ofisi za TAKUKURU Dodoma baada ya kuhojiwa. Masauni ni miongoni mwa viongozi wanaohojiwa kutokana na agizo la Rais Magufuli kuitaka Takukuru kuwahoji wale wote waliohusika na mkataba aliodai una harufu ya ufisadi

Masauni amefika Ofisini hapo muda mfupi baada ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima kumaliza kuhojiwa na kuondoka.

Jana Ijumaa Januari 31, 2020 Takukuru alihojiwa aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Kangi Lugola, Meja Jenerali Jacob Kingu (alikuwa katibu mkuu) pamoja na aliyekuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye.