Home Mchanganyiko HKUNA KATAZO KWA MTANZANIA ALIYEKO CHINA KUREJEA NYUMBANI

HKUNA KATAZO KWA MTANZANIA ALIYEKO CHINA KUREJEA NYUMBANI

0

Tanzania imesema hakuna katazo kwa Mtanzania yeyote aliyeko nje ya Nchi, China ikiwemo anayezuiwa kurudi Tanzania pindi atakapo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Mnyepe amewaondoa wasiwasi Watanzania hasa wale wanaotaka kusafiri kwenda ama kurudi kutoka China,na kwamba wale wanaotaka kusafiri kwenda China tayari waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ameshatoa maelekezo lakini kwa wale wanaotaka kurudi kutoka China Ubalozi wa Tanzania Nchini China unashirikiana nao kuwarejesha Tanzania kwa wale wanaotaka na kwamba hakuna katazo la kurejea Tanzania.