Mshambuliaji Leonel Messi akipongezwa na Arturo Vidal baada ya kuifungia Barcelona mabao mawili dakika za 59 na 89 katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Leganes kwenye mchezo wa Hatua ya 16 Bora Kombe la Mfalme Hispania usiku wa Alhamisi Uwanja wa Camp Nou. Mabao mengine ya Barca inayotinga Robo Fainali sasa, yamefungwa na Antoine Griezmann dakika ya nne, Clement Lenglet dakika ya 27 na Arthur Melo dakika ya 77 PICHA ZAIDI SOMA HAPA