Daktari wa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Amanda Anyoti akimwelezea balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Oded Joseph jinsi wanavyowahudumia watoto wenye matatizo ya moyo wakati balozi huyu alipotembelea JKCI jana kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.
Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Oded Joseph akimjulia hali mtoto Nembris Lubulo aliyelazwa katika wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Mhe. Balozi Joseph alitembelea Taasisi hiyo jana kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.
Daktari bingwa wa usingizi na wagonjwa walioko katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Faraji Lydenge akimsomea balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Oded Joseph taarifa ya mtoto anayefanyiwa upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo na kuzibwa tundu la moyo wakati balozi huyo alipotembelea chumba cha upasuaji. Mhe. Balozi Joseph alitembelea Taasisi hiyo jana kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Oded Joseph alipotembelea taasisi hiyo jana Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuona huduma mbalimbali za matibabu ya moyo zinazotolewa.
Picha na: JKCI