Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dar es salaam kilichokutana leo Januari 30,2020 katika Ofisi ya CCM Mkoa wa Dar es salaam Lumumba kwa ajili ya kujadili namna ya kuadhimisha miaka 43 ya kuzaliwa Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na utatuzi wa baadhi ya Changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa majukumu ya Chama pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi mwaka 2015, 2020.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar xes salaam Bibi Katwe Kamba alipowasili katika Ofisi ya CCM Mkoa wa Dar es salaam Lumumba leo Januari 30,2020 kwa ajili ya kuongoza kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Dar es salaam kilichojadili namna ya kuadhimisha miaka 43 ya kuzaliwa Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na utatuzi wa baadhi ya Changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa majukumu ya Chama pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi mwaka 2015, 2020. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
*******************************
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam na Pwani ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewataka Wajumbe wa Kamati za Siasa za Mikoa hiyo kutembelea na kuangalia maendeleo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Makamu wa Rais amesema hayo leo katika Ofisi ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam Lumumba wakati wa kikao cha kujadili namna ya kuadhimisha miaka 43 ya kuzaliwa Chama cha Mapinduzi CCM pamoja na utatuzi wa baadhi ya Changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa majukumu ya Chama pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi mwaka 2015, 2020 katika Mikoa ya Dar es salaam na Pwani.
Ambapo pia amekutana na baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Pwani katika Makazi yake Oysterbay Jijini Dar es salaam ambapo wamejadili kuhusu mradi wa Ujenzi wa Jengo la kitega Uchumi la Mkoa wa Pwani linalojengwa katika Eneo la Kibaha.
Amesema Serikali imetowa pesa kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi lakini bado kuna baadhi ya Watu wasio waaminifu wamekuwa wakizitumia vibaya pesa hizo na kusababisha kuchelewa kukamilika kwa baadhi ya miradi hiyo hivyo ni vyema wakaingia ndani kwa Wananchi ili kuweza kujionea uhalisia wa maendeleo ya miradi hiyo.
Nae Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es salaam akisoma Risala ya Mkoa huo amesema CCM Mkoa wa Dar es salaam kwa mwaka huu umeingiza jumla ya Wanachama wapya laki mbili elfu saba na mia mbili na Hamsini na sita.