…………………………………………………………………………………………
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema Tanzania inanufaika kiulinzi na usalama kutokana na kuwa mjumbe wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi wa nchi za ukanda wa Kusini mwa Afrika (SARPCCO).
IGP Sirro ameyasema hayo leo wakati alipokuwa akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kikao na Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Polisi Zimbabwe, TG Matanga ambaye yupo nchini kwa ziara maalum.
IGP Sirro amesema kuwa kutokana na kuwa mjumbe wa shirikisho hilo, Tanzania imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzuia na kudhibiti makosa yanayovuka mipaka yakiwemo makosa ya usafirishaji haramu wa binadamu, wizi wa magari na dawa za kulevya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho hilo ambaye pia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Zimbabwe, Kamishna Jenerali TG Matanga, amesema yupo nchini kwa ziara maalum ya kufanya tahmini ya utekelezaji wa maazimio ya INTERPOL pamoja na maazimio ya SARPCCO.