Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti (kushoto) akifurahia jambo na Mkuu wa Chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture muda mfupi kabla ya
kusaini utakayoiwezesha SBL kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa klimo wa chuo hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti (kushoto) akibadishana mkataba na Mkuu wa Chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture muda mfupi baada ya kusaini mkataba huo utakaiwezesha SBL kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa kilimo wa chuo hicho kila mwaka
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture watakaonufaika na mpango wa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa kilimo unaotolewa na Kampuni ya Bia ya Serengeri, wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti (kushoto) na mkuu wa chuo hicho Sinani Simba muda mfupi baada ya kusaini mkataba wa ufadhili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Ocitti (kulia) akimpongeza mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture ambaye ni mnufaika wa programu ya ufadhili wa elimu kwa wanafunzi wa kilimo Emmanuel Ntandu muda mfupi
baada ya SBL kusaini mkata wa ufadhili na chuo hicho mjini Bagamoyo jana.
******************************
Bagamoyo, January 29, 2020: Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), leo imezindua mpango wa ufadhili wa masomo utakaowanufaisha wanafunzi 30 kutoka katika jamii za wakulima hapa nchini kupata elimu ya ngazi ya chuo katika vyuo vya ndani vinavyofundisha masomo ya kilimo.
Ukijulikana kama Kilimo-Viwanda scholarship program, mpango huu unalenga kuongeza wataalamu wa kilimo watakaowasaidia wakulima nchini kuongeza uzalishaji, alisema Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Mark Ocitti wakati wa uzinduzi wa program hiyo katika chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani.
“Ni muhimu kwetu sisi kama SBL kuiunga mkono Serikali katika kuwajengea uwezo wakulima
wetu kupitia kuwaongezea wataalamu wa kilimo watakaosadia kuwashauri na hivyo kuongeza
tija katika kilimo,” alisema Ocitti.
Chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture ni moja kati ya vyuo vitatu ambavyo kampuni ya SBL inashirikiana navyo katika kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa kilimo hapa nchini.
Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa, programu hiyo inawalenga siyo tu wanafunzi wanaotoka
katika familia zenye vipato duni lakini pia wanafunzi wanaotoka katika jamii za wakulima katika
sehemu mbali mbali hapa nchini. Kila chuo kitapata nafasi ya kutoa wanafunzi 10 kila mwaka na
watakaolipiwa ada na SBL mpaka watakapomaliza masomo yao.
Kwa mujibu wa Ocitti, programu hiyo ni sehemu ya mkakati wa SBL wa kuongeza kiasi cha nafaka ambacho kampuni hiyo inanunua kwa ajili ya uzalishaji wa bia ambazo ni pamoja na mahindi, shayiri na mtama. Alisema, mwaka jana SBL ilinunua zaidi ya tani za ujazo 17,000 za
nafaka kutoka kwa wakulima wa ndani sawa na asilimia 70 ya mahitaji yake yote ya malighafi kwa mwaka.
“Kampuni ya SBL inalengo la kuongeza kiasi cha malighafi inayonunua kutoka kwa wakulima wa ndani hadi asilimia 85 kufikia mwaka 2020 na ndiyo maana tumeona umuhimu wa kusaidia kusomesha wataalamu wa kilimo ili wakafanye kazi ya kuboresha kilimo chetu. Kwa sasa
kampuni inanunua malighafi kutoka kwenye mtandao wenye wakulima 400 hapa nchini,”.
alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Kaole Wazazi College of Agriculture Sinani Simba aliishukuru kampuni ya SBL kwa kuja na wazo la kutoa ufadhili wa masomo ya kilimo na kuongeza kuwa ili kilimo kiwe cha tija wataalamu wengi wanahitajika.
“Tunayo Furaha kwa kuwa ufadhili huu unawalenga wanafunzi wanaotokea katika familia zenye
vipato duni ambao kama siyo msaada wa SBL, wasingeweza kupata fursa ya kuendelea na
masomo,” alisema