Na Mwandishi wetu, Katavi
Serikali mkoani Katavi imetenga eneo la zaidi ya hekta elfu nne kwa ajili ya mifugo kwa lengo la kuhakikisha mifugo inatunzwa katika hali bora ili kukidhi mahitaji ya viwanda vinavyotegemea malighafi zitokanazo na mifugo
Afisa Mifugo wa mkoa wa Katavi bwana Zidieli Mhando amesema wameweka mkakati wa kuhakikisha wanawaelimisha wafugaji mbinu za ufugaji bora
Bwana Mhando amesema kwa sasa wafugaji wanafuga kwa mazoea ambapo wanakuwa na mifugo mingi wakati maeneo ya malisho ni machache
Kwa upande wao baadhi ya wafugaji wamesifu uamuzi huo na kusema kuwa wakati mwingine wanachungia katika mapori yaliyotengwa kwa ajili ya kukosa maeneo ya malisho
“Tunalipa faini kubwa wakitkamata watu wa TFS tukiwa kwenye mapori, sasa kwa kutenga maeneo maalum ya kufugia watakuwa wametusaidia” alisema Mikidadi Mbuganzito ambaye ni mfugaji kutoka kijiji cha Itenka
Dokta Kejeri Jila ni Mkufunzi Mkuu wa Mifugo Wizara ya Mifugo na Uvuvi ametaja changamoto kadhaa zinazopelekea Tanzania kukosa soko la bidhaa za mifugo kuwa ni pamoja na magonjwa malimbali ya mifugo
Ametaja magonjwa hayo kuwa ni pamoja na ng’ombe kutupa mimba ambapo amewashauri wafugaji kupunguza mifugo ili kuweza kuwahudia vizuri