Kamanda wa Polisi Dodoma Girres Muroto,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo ofisini kwake wakati akitoa taarifa za matukio kwenye mkoa wake.
Kamanda wa Polisi Dodoma Girres Muroto,akionyesha vitu mbalimbali vilivyokamatwa katika matukio ya wizi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo ofisini kwake wakati akitoa taarifa za matukio kwenye mkoa wake.
…………………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limemkamata Boniface Mushi ambaye
ni mlinzi wa Ofisi za TANESCO baaada ya kuvunja ofisi za hizo
eneo la area D jijini Dodoma na kuiba kompyuta mpakato[Laptop].
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini
Dodoma,Kamanda wa Polisi mkoani hapa Girres Muroto amesema msako
mkubwa ulifanyika katika eneo hilo ambapo mlinzi wa kampuni binafsi
ya ulinzi QSS Deus Mushi alikamatwa katika eneo la wilaya ya
Kwimba Mkoani Mwanza baada ya kuiba laptop hiyo kutoka Dodoma katika
ofisi za TANESCO, za mradi wa miundombinu ya umeme shirikishi ya
nchi tatu ambazo ni Tanzania ,Kenya na Zambia.
Katika tukio jingine kamanda Muroto amesema katika Mtaa wa Kizota
jijini Dodoma alikamatwa Joshua Elisha [38] mlinzi wa Kampuni ya
ulinzi ya KK Security mkazi wa Kizota Mbuyuni akiwa na
Copresssor ya friji kubwa ambayo ni mali ya wizi aliyoiba baada ya
kuvunja store ya lindo .
Aidha,Kamanda Muroto amesema jeshi hilo limeokota Jumla ya pikipiki
nne katika maeneo tofauti zikiwa zimetelekezwa na wahalifu wakati wa
doria ambapo wenye pikipiki walikimbia baada ya kukurupushwa wakiwa
kwenye harakati za kufanya uhalifu na pikipiki hizo ni MC.813 CDH
Fekon nyekundu MC .128 CCQ BOXER nyekundu MC 857 CCU TVS nyekundu na
T. 967 CKK BOXER nyeusi ambapo imebainika kuwa ni Namba bandia.
Pia,Jeshi hilo limefanikiwa kukamata nyara za serikali huku likiwaasa
wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya wahalifu mbalimbali nchini
wakiwemo waendesha bodaboda nyakati za usiku.