Wachezaji wa Manchester United wakimpongeza Diogo Dalot baada ya kufunga bao la pili dakika ya 13 katika ushindi wa 6-0 dhidi ya wenyeji, Tranmere Rovers ya Daraja la Pili kwenye mchezo wa Raundi ya Nne Kombe la FA England leo Uwanja wa Prenton Park huko Birkenhead, Merseyside. Mabao mengine ya Man United yamefungwa na Harry Maguire dakika ya 10, Jesse Lingard dakika ya 16, Phil Jones dakika ya 41, Anthony Martial dakika ya 45 na Mason Greenwood kwa penalti dakika ya 56 PICHA ZAIDI SOMA HAPA