Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Bw. Matias Haule akitoa elimu ya maambukizi ya UKIMWI kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Viganga na Shule ya Sekondari Mnyakongo zilizoko nje kidogo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa jana Wilayani humo.
Mtaalam Mhamasishaji wa Masuala ya Ukimwi kutoka TACAIDS Bw. Simon Ngaweye akitoa elimu ya maambukizi ya UKIMWI kwa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Viganga na Shule ya Sekondari Mnyakongo zilizoko nje kidogo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa.
********************************
Na Mwandishi wetu Dodoma
Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii mefanya kampeini ya kujilinda na maambukizi ya UKIMWI kwa vijana wa bodaboda na wanafunzi wa Sekondari na shule za Msingi Wilayani Kongwa na kuwataka vijana hao kujilinda dhidi ya maambukizi hayo kwani takawimu zilizopo sasa zinaonesha maambukizi yanaongezeka kwa vijana walio katika umri wa miaka kati ya 18-24.
Akiongea na wazee pamoja na viongozi wa dini Wilayani Kongwa Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Matias Haule aliutaja ugonjwa wa UKIMWI kuwa ni tishio kwa vijana wa rika hiyo kwani maambukizi hayo kwa Siku yanawapata watu 200 kwa siku na katika idadi hiyo vijana ni 79 ambapo idadi ya wasichana peke yake wanaoambukizwa kwa siku ni 63 ukilinganisha na wavulana 14.
Bwana Haule aliwaambia viongozi hao wa dini pamoja na wazee kuwa ni kutokana na hali hiyo ya maambukizi Nchini Wizara imekuja na kampeini iitwayo Timiza Malengo ili kuwafanya vijana na wote Nchini kujilinda dhidi ya ugonjwa huo ili waweze kutimiza malengo ya kimaisha waliyojiwekea.
Mara baada ya kupokea taarifa hiyo Kiongozi wa Kanisa la Anglikani Wilayani Kongwa Mchungaji Luzineth Kingamkono alisema katika Kitabu cha Kutoka ambacho ni cha pili katika Biblia Sura ya Ishirini haya ya Saba mstari wa kumi nanne inasema usidhini kwa lengo la kukataza binadamu kutojihusisha zinaa kabla ya wakati.
Aidha kiongozi huyo wa kanisa hilo uku akiendelea kutumia kitabu hicho kitakatifu alisema katika Kitabu cha Wakolinto Sura ya saba inasema kwasababu ya zinaa kila mtu na awe na mke wake wake na kwa maana hiyo Mungu alipotoa amri hiyo katika zile amri kumi za Mungu alilenga kuwakataza wale walio tayari katika ndoa lakini pia kuwataka wale mbao hawajaoa wala kuolewa kusubiri wakati wao.
Aidha ni kwa mkutadha huo basi Kiongozi wa Baraza la Waislam Wilaya ya Kongwa Bw. Yahaya Said ameiomba Serikali kuacha kutoa vibari vya muziki kwa watoto yaani disko toto kwa kuwa haoni kama watoto wadogo wana kitu cha maana wanachojifunza kwa kuwepo disko toto katika jamii zaidi ya kuwaanda kupenda starehe katika maisha yao.
Pamoja na Wizara kukutana na wazee hao wa Wilaya ya Kongwa Wizara pia ilikutana na vijana wa Bodaboda wanaofanya kazi zao maeneo ya Kibaigwa kando ya barabara kuu iendayo Dodoma toka Dar es Salaam na kuwataka kujilinda na UKIMWI kufuatia magari kubwa ya biashara kutumia eneo hilo kutokana na uwepo wa Soko la Kimataifa la mahindi.
Mtoa mada za UKIMWI kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania TACAIDS Bw. Simon Ngaweye aliwataka vijana wa Boda boda kutokubali kushawishiwa kufanya ngono ili waweze kutimiza malengo yao ya kukua kibiashara na kuwataka kuamini inawezekana kuishi bila ukimwi endapo wataweza kujilinda.
Aidha Bw. Salim Ally Manyumba mfanyabiashara wa Kibaigwa Wilayani Kongwa ameiomba serikali kutoa elimu ya maambukizi ya UKIMWI kwa vijana wa boda boda kutokana na changamoto wanayaokutana nayo ya kurubuniwa na baadhi ya wanawake wanaotaka kujiridhisha kimapenzi kwa kuwa bodaboda ni rahisi kuingia katika mitego yao kutokana na wao kufanya biashara kwa karibu na vijana hao.
Wizara ya Afya Maendealeo ya Jamii kwa Kushirikiana na TACAIDS pamoja na Shirika la TASAF wako Mkoani Dodoma kutembelea wasichana barehe na wanawake vijana pamoja na Shule mbalimbali Mkoani humo kwa lengo la kuhamasisha vijana juu yatishio jipya la maambukizi ya UKIMWI kwa vijana na zoezi hili litaendelea kwa Mkoa wa Morogoro na baadae Nchi Nzima.