Muungano wa Waombaji kutoka Makanisa mbalimbali Shinyanga mjini, (Prayer Network Family) Wametembelea kaya zenye uhitaji zilipo katika Kijiji cha Lyandu Kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga, kwa kuziombea pamoja na kutoa msaada wa vitu mbalimbali.
Akizungumza mara baada ya watumishi hao wa Mungu kumaliza kutoa huduma hiyo kwenye Kaya zenye uhitaji Angelina Chediel, amesema wao wameguswa na familia hizo zenye uhitaji zilizopo katika kijiji hicho cha Lyandu, na kuamua kuzitembelea kwa kutoa neno la mungu pamoja na kuwapatia misaada mbalimbali.
“Napenda kutoa wito kwa jamii kwa wale ambao wenye nafasi , wajenge utamaduni wa kusaidia watu wenye uhitaji, leo katika kijiji hiki cha Lyandu tumetembelea Kaya Nne ambazo zina lea watoto wenye ulemavu, ambao wanakabiliwa na changamoto za kimaisha, na tumetoa kile ambacho tumejaliwa na Mungu,”amesema Chediel.
“Vitu ambavyo tumetoa kwenye familia hizi nne zenye uhitaji ni nguo, fedha, vyakula ambavyo ni Unga, mafuta ya kupikia, Sabuni, dawa za meno, viberiti, Chumvi, pamoja na msaada huu pia tumetoa neno la Mungu na kuzibariki Kaya hizi,”ameongeza.
Naye Muinjilisti Ester Emmanuel, ametoa wito kwa familia zile ambazo zinalea watoto wenye ulemavu mbalimbali, wasiwatenge na kuwanyanyapaa, bali wawapatie huduma za kimalezi kama walivyo watoto wengine ambao hawana ulemavu, ikiwamo na kuwapeleka kupata elimu kwenye shule za walemavu.
Nazo Kaya hizo zenye uhitaji zilizotembelea na kupewa msaada ikiwemo Kaya ya Bwana Thomas Musoma, wametoa shukrani kwa watumishi hao wa Mungu, kwa kuwapatia msaada pamoja na Neno la Mungu, huku wakitoa wito kwa watu wengine waige mfano huo wa kusaidia watu wenye uhitaji.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mwenyekiti wa Muungano wa waombaji kutoka Makanisa mbalimbali Angelina Chediel, akizungumza mara baada ya kumaliza kutoa huduma ya kiroho na msaada kwenye familia zenye uhitaji kutoka katika Kijiji cha Lyandu Kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga. Picha zote na Marco Maduhu – Malunde 1 blog
Wanakikundi kutoka Muungano wa waombaji kutoka makanisa mbalimbali Shinyanga mjini wakitoa msaada kwenye Kaya isiyojiweza Katika kijjiji hicho Cha Lyandu.
Mwenyekiti wa Muungano wa waombaji kutoka Makanisa mbalimbali Shinyanga mjini Angelina Chediel akitoa msaada kwa mtoto mwenye ulemavu mwenye uhitaji.
Mwinjilisti Ester Emmanuel akitoa msaada kwa mtoto mlemavu mwenye uhitaji.
Waombaji kutoka Makanisa mbalimbali Shinyanga mjini wakiendelea kutoa zawadi kwenye familia zenye uhitaji.

Muinjilisti Ester Emmanuel akitoa msaada kwenye familia yenye uhitaji.
Mtoto mwenye ulemavu George Thomasi akishukuru msaada ambao amepatiwa na watumishi hao wa Mungu.
Waombaji kutoka Makanisa mbalimbali Shinyanga mjini, (Prayer Network Family) awali wakiwasili kwenye Kaya yenye uhitaji katika kijiji cha Lyandu Kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kutoa msaada na kuziombea familia hizo.
Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog