Katibu Mkuu wa Chama Cha UPDP Hamad Moh’d Ibrahim akiwasisitiza Wananchi wa Zanzibar kujiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura wakati wa mkutano na Waandishi wa habari katika Ukumbi wa Rahaleo.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama TLP Taifa , Zanzibar Hussein Juma Salum akijibu maswali mbali mbali yaliyoulizwa na Waandishi wa Habari huko Ukumbi wa Rahaleo katika Kikao cha Viongozi wa Vyama vya siasa Tanzania Pamoja na Waandishi hao.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakiskiliza Tamko la Viongozi wa Vyama vya Siasa Tanzania la kumpongeza Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kwa mafanikio makubwa katika uongozi wake wa miaka tisa katika ukumbi wa Sana Rahaleo Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia Makini Ameir Hassan Ameir akitoa Tamko la Viongozi wa Vyama kumi vya Siasa Tanzania la kupongeza mafanikioya miaka tisa ya Uongozi wa Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraa la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Mjini Zanzibar.
Picha Na Maryam Kidiko / Maelezo Zanzibar.
******************************
Na Kijakazi Abdalla Maelezo 25/01/2020
Viongozi wa Vyama 10 vya Siasa Tanzania wamempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein kwa kutimiza miaka tisa ya uongozi pamoja na kufanikisha vyema sherehe za miaka 56 ya Mapinduzi Zanzibar.
Akitoa pongezi hizo kwa niaba ya vyama hivyo Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia Makini Ameir Hassan Ameir wakati akizungumza na Waandishi wa Habari huko katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo.
Amesema pongezi hizo kwa Rais wa Zanzibar zinatokana kuwa na mafanikio makubwa yaliyopatikana ya maendeleo ikiwemo kuimarika kwa amani na utulivu katika nchi.
Aidha amesema katika kipindi cha uongozi wa Dkt Shein vyama vya siasa vimeweza kushuhudia kuimarika kwa demokrasia kwa kupatiwa nafasi ya kushiriki katika kuunda Serikali pamoja na kuongoza Wizara.
Alisema katika kuleta maendeleo ya nchi Uchumi wa Zanzibar umekuwa kutoka kwa asilimia 4.3 hadi kufikia 7.1 hatua ambayo imeweza kuondosha utegemezi wa bajeti .
Aidha wamempongeza kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato kwa ZRB pamoja na TRA kwa kutekeleza vizuri majukumu yao ambapo hali hiyo inaweza kuwavutia wawekezaji kuekeza Zanzibar na kuongeza ajira kwa Wananchi.
Hata hivyo wamesema katika kipindi cha miaka tisa ya Uongozi wa Dkt Shein kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali bajeti kuongezwa kwa vipindi 3 hali hiyo imeweza kuleta fikra za kuendeleza elimu bure kuanzia maandalizi hadi sekondari pamoja na kufuta ada zote ambazo wazazi walizokuwa wakitozwa.
Aidha wamesema katika kuimarika miundo mbinu ya makazi bora wananchi wa Zanzibar ikiwa ni utekelezaji wa ahadi za Mapinduzi Zanzibar ya mwaka 1964 pamoja na kuanza kwa ujenzi wa nyumba mpya za Kwahani.
Hata hivyo wapinzani hao wamewataka wananchi wote wenye sifa za kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ambalo litawawezesha kushiriki katika uchaguzi Mkuu ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba 2020 mwaka huu wajitokeze kwa wingi.
Tamko hilo la pongezi limetolewa na viongozi wa vyama vya upinzani ,vyama vyenyewe ni Chama cha Demokrasia Makini,Ada-Tadea,TLP.NLD,DP,SAU,UPDP,AFP,ADC, na NCCR-Mageuzi .