Simba SC imetinga hatua ya 16 ya kombe la Shirikisho baada ya kuichapa mabao 2-1 Mwadui FC huku ikilipa kisasi cha kupigwa mabao moja mechi ya Ligi Kuu mchezo uliomalizika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mwadui FC walikuwa wa kwanza kuwashangaza mashabiki wa Simba dakika ya 34 kupitia kwa Gerald Mdamu akimalizia pasi ya Ludovick.
Mchezaji wa kimataifa kutoka Zambia Clatous Chama aliwarejesha mchezoni wachezaji wa Simba kwa kufunga bao maridadi akiwa nje ya 18 dakika ya 45+2.
Shujaa wa Simba ni kiungo hatari Francis Kahata aliwanyanyua mashabiki kwa kufunga bao la ushindi dakika 84 akimalizia pasi ya Kapombe na kuiwezesha timu yake kusonga mbele kwa ushindi wa 2-1
Michuano hiyo itarajia kuendelea kesho katika uwanja huo huo wa Taifa Yanga itamenyana na wageni Tanzania Prisons mchezo unaptabiriwa kuwa mgumu kwa pande zote mbili