Home Mchanganyiko PWANI YAOMBA ONGEZEKO LA MITA 4,500 ZA WATEJA WAPYA KUPITIA REA III-MGALU

PWANI YAOMBA ONGEZEKO LA MITA 4,500 ZA WATEJA WAPYA KUPITIA REA III-MGALU

0
NA MWAMVUA MWINYI,KISARAWE
WIZARA YA NISHATI imepokea ombi la Shirika la Umeme (TANESCO ) Mkoani Pwani la ongezeko la mita 4,500 kwa ajili ya wateja wapya ambazo hazikuwepo katika wateja 5,300 waliopangwa kuunganishwa kupitia mradi wa REA awamu ya III mkoani hapo.
Kutokana na mkoa kuwa bado na mahitaji makubwa, ombi hilo limeshaidhinishwa na bodi ya wakurugenzi wa REA .
Naibu Waziri Wa Nishati, Subira Mgalu aliyasema hayo, wakati akiwa kwenye ziara ya ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani,ambapo alisema kwasasa REA inashughulika na manunuzi ya mita hizo za ziada na kisha zitakabidhiwa Tanesco ama kwa mkandarasi .
“Maombi haya ni karibu mikoa yote kadri mahitaji yanavyoongezeka ,”:miradi ya aina hiyo inapotekelezwa kuna kuwa na wigo na idadi ya wateja na mkoa huo awali ulipangwa kuunganishiwa wateja 5,300 “alisema Subira.
Alieleza, asilimia 90 ya wateja hao walishaunganishiwa lakini mahitaji bado ni makubwa .
 
Hata hivyo, Subira alieleza kwa Kisarawe wateja 239 walishalipia lakini wameshindwa kuunganishwa kwa wakati .
 
Alibainisha, wananchi wote ambao wamelipia huduma ya umeme wa REA III mzunguko wa kwanza ambao kwenye idadi ya wateja wa awali walikuwa wamezidi idadi iliyopo kwenye mkataba wa mradi huo  na kushindwa kuunganishiwa umeme kuwa wataunganishiwa na huduma hiyo.
“Kisarawe wapo wananchi 239 walishalipa lakini walishindwa kuunganishwa kwa wakati kwasababu idadi iliyohitajika kwa kisarawe ilishakamilika kwahiyo sasa niwatoe hofu wote waliolipa na ambao hawajalipa kwamba unganishaji umeme utaanza na sasaivi REA wapo kwenye manunuzi ya vifaa”
Subira akielezea mradi wa umeme wa Peri-Urban Naibu Waziri huyo alisema, mradi umebuniwa kwa mara ya kwanza nchini ili kukidhi haja ya ongezeko la mahitaji ya umeme kwa maeneo ambayo yanakuwa kwa kasi.
Pia  utasaidia serikali kufikia lengo lake la kuwa ifikapo June 2021 vijjiji vyote viwe vimeunganishwa  umeme na Wizara inamatumani makubwa kuwa lengo hilo litafikiwa kwa kupitia miradi mbalimbali kama REA 111, Peri-Urban na Ujazilizi.
Nae mkuu wa wilaya  ya Kisarawe Jokate Mwegelo aliipongeza serikali ya awamu kwa kuwafikishia umeme wananchi wa Kisarawe ambao awali walikuwa wakililia kupata umeme na wengine kutumia vibatari na solar.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Kisarawe , Hamis Dipakutile alieleza changamoto ya baadhi ya maeneo umeme haujafika ila anaimani kwa juhudi za Tanesco Pwani na wizara ya nishati umeme utafika na mradi huo utakuwa mkombozi kwa wananchi kuinua maendeleo.