Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine akifungua semina iliyoandaliwa na Ofisi hiyo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira leo Januari 25, 2020 jijini Dodoma ya kuwajengea uwezo kuhusu mada mbalimbali zikiwemo Umuhimu wa uhandisi jeni katika kuongeza tija katika kilimo, Fursa za teknolojia ya kisasa kwenye afya, Usimamizi wa matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa na Matumizi ya bioteknolojia ya kisasa kwa maendeleo ya mifugo na afya, fursa na changamoto zake. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira katika Ofisi hiyo, Faraja Ngerageza.
Mhadhiri Idara ya Biolojia ya Molekyuli na Bayoteknolojia Ndaki ya Sayansi Asilia na Tumizi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Daniel Maeda akiwasilisha mada Matumizi ya bioteknolojia ya kisasa kwa maendeleo ya mifugo na afya, fursa na changamoto zake katika semina kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira iliyofanyika leo jijini Dodoma na kuandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Afisa Mazingira Mwandamizi Ofisi ya Makamu wa Rais, Thomas Chali akitoa mada kuhusu Usimamizi wa matumizi salama ya biotechnolojia ya kisasa katika semina kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira iliyofanyika leo jijini Dodoma na kuandaliwa na Ofisi hiyo.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira wakiwa katika semina kuhusu Umuhimu wa uhandisi jeni katika kuongeza tija katika kilimo, Fursa za teknolojia ya kisasa kwenye afya, Usimamizi wa matumizi salama ya biotechnolojia ya kisasa na Matumizi ya bioteknolojia ya kisasa kwa maendeleo ya mifugo na afya, fursa na changamoto zake kilkiyofanyika jijini Dodoma na kuandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Sehemu hiya wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wakifuatilia semina iliyoandaliwa kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)