Wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa tamasha hilo,Dave Ojay ,katikati ni Mwenyekiti wa bodi ya chuo hicho Dokta Servacius Likwelile na anayefuata ni Mkurugenzi mkuu wa chuo hicho ,Ezra Mbogori wakati wakizungumza na waandishi wa habari Leo jijini Arusha(Happy Lazaro).
Mkurugenzi mkuu wa chuo hicho Cha MS-TCDC,Ezra Mbogori akizungumza na waandishi wa habari katika tamasha la Sanaa linalofanyika chuoni hapo.(Happy Lazaro).
*********************************
Happy Lazaro,Arusha.
Arusha,Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuhudhuria katika tamasha la sanaa na ufahamu (Kan Festival)ili kuweza kuongeza ujuzi na maswala ya maendeleo katika kukuza na kuinua uchumi wao.
Tamasha hilo ambalo linaendelea katika chuo cha maendeleo na ushirikiano wa kimataifa (MS-TCDC )mkoani Arusha kwa muda wa siku nne linalenga kubadilisha fikra za watu mbalimbali na kuweza kuwaza maswala ya maendeleo .
Hayo yamesemwa leo jijini Arusha na Mkurugenzi mkuu wa chuo hicho ,Ezra Mbogori wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi hayo ambayo yanaendelea chuoni hapo.
Amesema kuwa,tamasha hilo mbali na kuwepo kwa burudani kutoka kwa wanamuziki mbalimbali linalenga pia kubadilisha fikra za watu ,hivyo kuwataka wanafunzi wa vyuo kuitumia fursa hiyo kwa ajili ya kujifunza maswala mbalimbali kwa wenzao kutoka nje ya nchi.
“Tunawaomba Sana watu mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa vyuo wajitokeze kwa wingi kuja kutumia fursa hiyo katika kujifunza maswala mbalimbali na kujionea Sanaa za wenzetu kutoka nje ya nchi na kupata uzoefu wa kutosha kutoka kwao”amesema Mbogori.
Mwenyekiti wa bodi ya chuo hicho,Dokta Servacius Likwelile amesema kuwa kupitia tamasha hilo ni fursa pekee kwao kuweza kubadilishana utaalamu,ujuzi,Sanaa na kujenga Mtandao zaidi kwani tamasha Kama Hilo hutokea Mara moja kwa mwaka.
Amesema kuwa,Sanaa ina nafasi kubwa Sana katika kubadilisha hisia za watu na kufikisha ujumbe hivyo baada ya tamasha hilo wanatarajia kuwepo kwa idadi kubwa ya watu watakaoweza kubadilika kifikra na kuweza kuchochea swala zima la maendeleo katika maeneo yao.
Mkurugenzi wa tamasha hilo,Dave Ojay amesema kuwa,kauli mbiu katika tamasha hilo ni ‘maendeleo ni watu na sio vitu”maneno ambayo yalikuwa yakitumiwa Sana na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ,hivyo kupitia tamasha wanazidi pia kumuenzi Mwalimu Nyerere.
Ojay amesema kuwa,nje ya burudani lakini pia watakuwa na kipindi Cha mazungumzo yanayobadilisha maisha ya watu kitakachoenda na burudani mbalimbali ambazo zitakuwa zimebeba ujumbe wenye lengo la kuelimisha.
Ojay amesema kuwa ,tamasha hilo limehudhuriwa na wageni zaidi ya 5,000 kutoka nchi Saba ndani na nje ya nchi na Ni tamasha la pili kufanyika chuoni hapo.
Ametaja wanamuziki wanaoshiriki katika tamasha hilo kuwa ni mwanamuziki kutoka nchini Tanzania ,Fid Q,Vitali Maembe ,Sandra Nankoma kutoka Uganda ,Juma Tutu kutoka Kenya ,Victor Kunonga kutoka Zimbabwe,Isabella Novela kutoka Mozambique .
Hata hivyo nchi zinazoshiriki tamasha hilo ni pamoja na Kenya,Tanzania,Uganda, Mozambique,Burundi, Zimbabwe,Afrika Kusini na Congo.