Mratibu wa Mpango wa Elimu Changamani kwa Vijana Walio Nje ya Mfumo Rasmi wa Elimu (IPOSA) kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Dkt. Sempeho Siafu (alishika randa) akitoa maelezo kwa walimu wa Shule za Msingi nne za Wilaya ya Kaliua ambao walikuwa wakihudhuria mafunzo ya siku 14 kuhusu ujasiriamali na ufundi.
Katibu Tawala Wilaya ya Kaliua Michael Nyahinga (katikati) akitoa maelezo kwa walimu wakati alipokuwa akitembelea maonesho ya bidhaa zilizozalishwa na walimu wa shule za Msingi nne waliokuwa wakihudhuria mafunzo ya ujasiriamali na ufundi chini ya Mpango wa Elimu Changamani kwa Vijana Walio Nje ya Mfumo Rasmi wa Elimu (IPOSA)
Mmoja wa walengwa wa Mpango wa Elimu Changamani kwa Vijana Walio Nje ya Mfumo Rasmi wa Elimu (IPOSA) kutoka Wilaya ya Kaliua Josia Silas akitoa maelezo kwa Katibu Tawala wilaya ya Kaliua Michael Nyahinga (mwenye suti nyeusi katikati) kuhusu mafunzo ya ushonaji aliyopata chini ya mpango huo.
……………..
WALIMU 16 wa wilaya ya Kaliua waliopata mafunzo juu ya utekelezaji wa Mpango wa Elimu Changamani kwa Vijana Walio Nje ya Mfumo Rasmi wa Elimu (IPOSA)wametakiwa kuhakikisha elimu waliyopata ianawafikia walengwa wote kama ilivyokusudiwa .
Kaliu hiyo imetolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Kaliua Michael Nyahinga wakati akifunga mafunzo ya wiki mbili ya walimu kutoka Shule za Msingi nne zinazotekeleza Mpango wa IPOSA.
Alisema elimu walipata kutolewa kwa moyo na weledi bila ubaguzi wa namna yoyote ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kuondoa ujinga na kujenga uchumi wa Kati ambao msingi wake mkuu ni Viwanda.
Nyahinga alisema walimu hao wakitekeleza kwa weledi jukumu lako watalisaidia kundi hilo ambalo lilikuwa nje ya mfumo rasmi wa elimu kupata maendeleo na jamii inayowazunguka katika kuanzisha vikundi vya uzalishaji mali.
Meneja wa SIDO Mkoa wa Tabora Samwel Neligwa alisema watoa mafunzo mbalimbali kwa walimu wa IPOSA kama vile ufundi, utengenezaji wa bidhaa mbalimbali ili nao waweze kueneza ujuzi huo kwa vijana waliopo chini ya mpango wa IPOSA.
Alisema vijana hao wakifaulu vizuri watasaidia jitihada za Serikali za uzalishaji wa viwanda ikiwemo vidogo vodogo baada ya kuunganishwa katika vikundi vya uzalishaji mali.
Naye Mwalimu wa Shule ya Msingi Kaliua Kituo cha IPOSA Ramadhan Jalala aliasema mafunzo waliopatiwa yatawawezesha kuwasaidia watoto ambao hawakupitia katika mfumo rasmi kupata elimu ya ujasirimali na ufundi na kuwafanya wajitegemee.
Aliiomba Serikali kuhakikisha elimu hiyo inapelekwa katika Mikoa yote nchini ili kuwawezesha watoto wengi ambao wako nje ya mfumo rasmi wa elimu kupata ujuzi wa maeneo mbalimbali.
Mratibu wa IPOSA kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Dkt. Sempeho Siafu alisema utafiti uliofanyaika ulibaini kuwa kuna jumla ya watoto milioni 3.5 wako nje ya mfumo rasmi wa elimu
Alisema Mpango wa Elimu Changamani unalenga kuwajengea uwezo vijana ambao wako nje ya mfumo wa elimu katika maeneo ya ufundi ya ujasiriamali ili waweze kuanzisha viwanda vidogo vidogo.
Dkt. Siafu alisema vijana hao wataunganishwa katika vikundi na kupatiwa mikopo inayotolewa na Halmashauri kwa ajili ya uzalishaji mali na kuendeleza vikundi vyao