Ujenzi wa matundu ya vyoo 9 katika shule ya mzingi Namunda uliokuwa umekwama, umeanza kutekelezwa baada ya Gavana Shilatu kutoa saa 24
………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu Mihambwe
Hatimaye ujenzi uliokuwa umekwama kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa kutokana na uzembe, mivutano umeanza kama ulivyoagizwa uanze ndani ya saa 24.
Ujenzi huo ni wa vyoo matundu 9 katika Shule ya Msingi ya Namunda iliyopo kata ya Kitama ambao Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu alitembelea na kukuta umekwama na kuagiza uanze mara moja ndani ya saa 24.
Gavana Shilatu alifika shuleni hapo kujionea utekelezaji wa agizo lake na kukuta shimo likiwa hatua ya mwishoni kumaliziwa kuchimbwa tayari kuanza kulijengea.
Mara baada ya kupewa taarifa ya ujenzi wa mradi huo ulivyofika mpaka sasa, Gavana Shilatu alisisitiza kasi ya ujenzi iongezwe zaidi.
“Niwapongeza kwa kuanza uchimbaji shimo. Nasisitiza tuongeze kasi zaidi, vyoo vikamilike mapema na vianze kutumika, tumechelewa sana.” Alisisitiza Gavana Shilatu.
Katika ziara hiyo Gavana Shilatu aliambatana na halmashauri ya Serikali ya Kijiji, Kamati ya ujenzi na uongozi wa shule.