*******************************
KAMA MNAVYOFAHAMU, LAINI ZA SIMU AMBAZO
HAZIJASAJILIWA KWA KUTUMIA NAMBA YA KITAMBUSHO CHA TAIFA (NIDA) NA KUTHIBITISHWA KWA ALAMA ZA VIDOLE ZILIANZA KUZIMWA TAREHE 20 JANUARI, 2020 USIKU NA ZOEZI LINAENDELEA.
HAKIKI TENA USAJILI WA LAINI ZAKO KWA KUPIGA NAMBA *106# NA UCHUKUE HATUA STAHIKI SASA.
1.0 KWA WALIOSITISHIWA HUDUMA ZA LAINI ZAO ZA SIMU
KUANZIA TAREHE 20.01.2020 WANAWEZA PIA
KUENDELEA NA UTARATIBU WA USAJILI KWA LENGO LA
AMA KURUDISHA LAINI ZAO ZILIZOFUNGWA KAMA
ZITAKUWA BADO ZIPO AU KUPATA LAINI MPYA. ZOEZI
HILI NI ENDELEVU.
2.0 KWA WATUMIAJI/WAOMBAJI (WATANZANIA) WAPYA WA LAINI ZA SIMU WATAENDELEA KUSAJILIWA MUDA WOTE KWA KUTUMIA KITAMBULISHO CHA TAIFA NA
KUHAKIKIWA KWA ALAMA ZA VIDOLE. HUDUMA HIYO NI
ENDELEVU PIA. 3.0 MATUMIZI SAHIHI YA VITAMBULISHO WAKATI WA USAJILI WA LAINI ZA SIMU (ZINAZOTUMIKA AMA KWA AJILI YA MAWASILIANO YA SIMU ZA SAUTI AU VIFAA VYA MAWASILIANO MENGINE) UKO KATIKA MAKUNDI YAFUATAYO:-
3.1 Sisi wa-Tanzania kitambulisho chetu ni kile cha Taifa
kitolewacho na NIDA kwa vigezo vyao;
ISO 9001:2015 CERTIFIED
3.2 Kwa wageni wanaokaa hapa nchini chini ya miezi
sita wanasajili laini za simu kwa kutumia namba za
Hati zao za kusafiria na kuhakiki kwa alama za vidole;
3.3 Kwa wageni wanaokaa zaidi miezi sita wanatumia
vitambulisho (Legal Resident ID) ambavyo hupewa
na NIDA (Hii ni kwa mujibu wa utaratibu wa Uhamiaji
na NIDA);
3.4 Kwa wanadiplomasia wanatumia Hati zao za kusafiria
pamoja na vitambulisho vyao vinavyotolewa na Wizara
ya Mambo ya nje; na
3.5 Kwa wakimbizi wanatumia vitambulisho vyao
ambavyo hupewa na NIDA (Hii ni kwa mujibu wa
utaratibu wa Uhamiaji na NIDA),
4.0 KATIKA KUJIRIDHISHA KUWA WALIOSAJILI LAINI ZAO ZA
SIMU WAMETUMIA VITAMBULISHO SAHIHI, TCRA KWA
KUSHIRIKIANA NA WATOA HUDUMA ITAFANYA ZOEZI LA
KUHAKIKI LAINI ZOTE ZITAKAZOKUWA ZIMESAJILIWA ILI
KUWAONDOA WALE WALIOSAJILI LAINI ZAO AMA KWA
KUTUMIA VITAMBULISHO VYA WATU WENGINE AU KWA
KUTUMIA KITAMBULISHO TOFAUTI SAMBAMBA NA
KUWACHUKULIA HATUA ZA KISHERIA.
5.0 IKUMBUKWE PIA KWAMBA KUSAJILI LAINI YA SIMU KWA KUTUMIA KITAMBULISHO CHA MTU MWINGINE NI KOSA SANJARI NA KUPEWA LAINI ILIYOSAJILIWA NA MTU
MWINGINE.
6.0 ONYO NA TAHADHARI ZINAENDELEA KUTOLEWA KWA
MAKUNDI YOTE YALIYOORODHESHWA KWENYE
KIPENGELE CHA 3.0 HAPO JUU, KUTOTUMIA
KITAMBULISHO KISICHOKUHUSU WAKATI UNASAJILI
LAINI ZAKO ZA SIMU (ZINAZOTUMIKA AMA KWA AJILI YA
MAWASILIANO YA SIMU ZA SAUTI AU VIFAA VYA
MAWASILIANO MENGINE).