Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiongea na wananchi wa Ngobanya kata ya Kimbiji,Wilaya ya Kigamboni, Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa ziara ya ukaguzi wa kazi ya kusambazaji umeme Mkoani humo.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiongea na watalaam mbambali wa Shirika la Umeme Tanzania mara baada ya kufanya ukaguzi wa kazi ya kusambazaji umeme katika mtaa wa Ngobanya kata ya Kimbiji,Wilaya ya Kigamboni, Mkoa wa Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika katika mkutano wa hadhara katika Mtaa wa Kitonga kata ya Msongala Wilaya ya Ilala Mkoani Dar es Saalam.
Wananchi wa Mtaa wa Kitonga, kata ya Msongala Wilaya ya Ilala Mkoani Dar es Saalam wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu( hayupo pichani) katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mtaa huo hapo.
*****************************
Hafsa Omar- Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amesema Serikali haitamuongezea Mda Mkandarasi wa kampuni ya Namis anaye tekeleza Mradi wa Peri-Urban katika jimbo la Ukonga jijini Dar es Saalam.
Aliyasema hayo, Januari 22 mwaka huu, wakati alipokuwa akijibu hoja mbalimbali za wananchi wa Mtaa wa Kitonga, Kata ya Msongala, wilaya ya Ilala, Mkoani Dar es Salaam, wakati akiwa kwenye ziara ya ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme mkoani humo.
Alisema, kuwa walimpa mradi huo mkandarasi huyo baada ya kushinda vigezo ambavyo vilihitajika wakati wa mchakato wa kutafuta mkandarasi kwenye mradi huo, na manatarajio yao atakamilisha mradi huo ndani ya mda uliopangwa ambao ni Mei mwaka huu.
“Niwatoe hofu na mtuamini kuwa tutakuja kuwasha umeme hapa Mei katika maeneo yote tena kwa mpigo, tunataka vitendo, Mkandarasi tunakuomba ufanye kazi usiku na mchana, hatutaki tena kuja kusikiliza kero za mradi huu imetosha”
Aidha,alisema Mkoa wa Dar es Saalam inauhitaji makubwa wa umeme, wananchi wapo tayari kupokea huduma hiyo muda wowote, na Serikali imejipanga kikamilifu kusambaza umeme kwenye jiji hilo na maeneo mengine yote nchini.
Alifafanua kuwa, sheria iliyounda Wakala wa Nishati vijijini(REA) ilipewa majukumu ya kusambaza umeme vijijini tu, lakini Serikali kwa kuona umuhimu wa kusambaza umeme kwenye maeneo ambayo yapo kwenye manispaa, ambayo sio mji au kijiji ikakumua kuleta mradi huo wa Peri-Urban ili nao wapate huduma ya umeme kwa bei ya 27,000 tu.
Pia, amelitaka Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) kuendelea kutafuta wateja kwa njia ya kuwaunganishia umeme wateja wengi ili Shirika liweze kutoa huduma kwa ufanisi na kujipatia mapato kupitia wateja hao .
Alieleza kuwa, Tanzania ndio nchi ya kwanza kwa Afrika Mashariki kwa usambazaji umeme, na imefakiwa kwa kiasi kikubwa kupeleka umeme vijijini na takribani vijiji vingi nchini tayari vimeshapatiwa umeme.
Aliongeza kuwa,dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kila kaya inapata Nishati, kwakuwa nishati ni maendeleo,na Wizara imejipanga kusambaza Nishati umeme na gesi, na tayari kazi ya usambazaji gesi majumbani imeanza katika maeneo ambayo bomba la gesi lilipopita na katika maeneo mengine ya nchini.
Katika ziara yake hiyo, Mkoani Dar es Saalam Naibu Waziri wa Nishati pia alikagua mradi wa Peri-Urban katika mtaa wa Ngombani kata ya kimbiji katika Wilaya ya Kigamboni.