Mfugaji ameiomba wizara ya Mifugo na Uvuvi mafunzo rejea ya Mifugo kwa Wafugaji na Maafisa Ugani kuleta mara kwa mara ili yaweze kuwasaidia pamoja na kupata Elimu zaidi.
Hivyo kutawasidia katika kuboresha shughuli za ufugaji wenye tija endelevu ya kuzalisha mifugo na malighafi ya kutoka ili kuweza kufikia uchumi wa kati wa viwanda.
Wito huo umetolewa Mkoani Katavi na mfugaji kutoka kijiji cha Katambike Halmashauri ya Nsimbo Bw,Shadadi Amrani wakati wa mafunzo rejea ya wafugaji huku akiishukuru Wizara kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo yawewasiadia kupata elimu na uelewa zaidi.
”Sisi kama wafugaji tunashukuru sana wizara kwa kuandaa haya mafunzo ambayo yametuoa eimu itakayokwenda kutusaidia katika shughuli za ufugaji ili tuweze kuboresha ufugaji uliobora na wenye tija kwetu”amesema Bw.Amrani
Aidha amesema kuwa mafunzo hayo yameweza kuwapa elimu ya kujua na kufahamu zaidi ufugaji wenye tija na wenye malengo ya kufikia uchumi wa kati hivyo watatumia kuboresha uzalishaji wenye tija.