Waziri wa Maji Mhe.Prof.Makame Mbarawa,akizungumza na watumishi wa wizara hiyo wakati wa uzindua Bodi Mpya ya Wakurugenzi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) hafla hiyo imefanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Wakurugenzi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) leo jijini Dodoma.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi ,akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Dkt.Binilith Mahenge kwenye uzinduzi wa Bodi Mpya ya Wakurugenzi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) leo jijini Dodoma.
Sehemu ya watumishi wa wizara ya maji wakifatilia hotuba ya Waziri Prof.Makame Mbarawa wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Wakurugenzi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) leo jijini Dodoma.
Waziri wa Maji Mhe.Prof.Makame Mbarawa,akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Wakurugenzi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) leo jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji Mhe.Mahmoud Mgimwa,akiongea wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Wakurugenzi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) leo jijini Dodoma.
Waziri wa Maji Mhe.Prof.Makame Mbarawa,akipeana mkono na Mwenyekiti wa Bodi ya RUWASA Pfor.Idris Mshoro mara baada ya kuzinduzi wa Bodi Mpya ya Wakurugenzi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) leo jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya RUWASA Pfor.Idris Mshoro,akionyesha ripoti mpya ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya Wakurugenzi wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) leo jijini Dodoma mara baada ya kuzinduliwa na Waziri wa Maji Prof.Makame Mbarawa.
…………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa imeitaka bodi mpya ya mamlaka ya Maji Safi na usafi wa Mazingira vijijini RUWASA kuhakikisha inakwenda kuondoa changamoto zilizopo ndani ya Mamlaka hiyo ili kuhakikisha malengo ya Serikali ya kuanzisha Wakala huo inakamilika na wananchi wa vijijini wanapata huduma ya maji Safi.
Wakati wa kuzindua bodi hiyo mpya Waziri Mbarawa amesema Wakala huo umeundwa ili kuondoa changamoto zote zilizopo katika Mamlaka hiyo na kuhakikisha malengo ya yanatimia ya kuhakikisha wananchi hasa wa vijijini wanapata huduma ya maji Safi.
“Tatizo la huduma ya maji Safi vijijini ni kubwa niwape changamoto bodi mpya mkahakikishe changamoto hizo zinatatuliwa hasa tatizo la miradi mingi kutokamilika kwa wakati” amesema.
Profesa Mbarawa amesema kumekuwa na madudu mengi ambayo yakifanywa na watendaji katika utendaji wao wa kila siku jambo ambalo halikubaliki kabisa.
Amesema uzinduzi wa bodi hii ukawe chachu ya kuifanya RUWASA iwe mfano wa kuigwa na bodi nyingine katika utendaji kazi zao za kila siku.
“Naamini bodi hii itakwenda kufanya mabadiliko makubwa na ndio bodi ya kwanza kuzinduliwa katika Mamlaka hii, “amesema.
Kuhusu kuanza kutumia force acaunt kwa baadhi ya miradi amesema imeanza kuleta matokeo mazuri kwani Kuna miradi imejengwa kwa fedha ndogo tofauti na wangetumia wakandarasi kitekeleza miradi hiyo.
“Watu hawaipendi force account kwasababu ya maslahi yao binafsi hivyo basi mwelekeo wa Wizara tutaanza kutumia kwenye miradi mingi kwani umeonyesha mafanikio. amesema.
Naye Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema wataalamu wanapaswa kuelekeza nguvu zao vijijini ili kutatua changamoto za maji zilizopo katika sekta ya maji.
Amesema watu wa vijijini wamekuwa wakipata shida ya maji na kunywa maji wanayokunywa ambayo pia hutumiwa na wanyama.
“Naomba wataalamu mtumie ujuzi mliopata ili kuokoa tatizo la maji hatupendi kusikia kila kukicha shida ya maji,”amesema Aweso.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa bodi ya RUWASA profesa Idriss Mshoro amesema bodi yao iko tayari kutekeleza kile walichoagizwa ili jamii iweze kupata maji.
Amesema anashkuru Rais Dk John Magufuli kwa kumteua katika nafasi hiyo ambayo amesema ataitendea haki.
Wakati Katibu wa Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo amesema wameanzisha mamlaka hiyo ili kutatua changamoto za maji vijijini hivyo watendaji wanapaswa kuwajibika.
Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa bodi hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya RUWASA, Prof Idris Mshoro ameipongeza serikali kwa ruzuku na msaada inayotoa kwa hivyo anaamini kwa uwekezaji ambao unafanywa changamoto ya maji nchini inakwenda kumalizika ndani ya kipindi kifupi.
” Sisi kama bodi tunaahidi kufanya kazi kwa uzalendo tukisimamia wakala huu uadilifu, uwajibikaji na bidii kwa kuhakikisha wote wanaofanya kazi na watakaopewa kazi za maji ni wale tu wenye sifa na vigezo na siyo vinginevyo,” Amesema Prof Mshoro.