Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza akizungumza naWadau wa Filamu mkoa waSingida jana.
Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza (wa tatu kulia) akisikiliza maoni na changamoto kutoka kwa wadau wa filamu mkoani Singidajana. Wa kwanza kulia ni Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Singida, Henry Kapella, Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Dkt. Kiagho Kilonzo.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Na Godwin Myovela, Singida
HATIMAYE Serikali imepata majawabu yatakayo saidia kupunguza changamoto sugu za wa sanii nchini, ikiwemo tatizo la muda mrefu la ‘ukata’ wamaisha na mitaji duni katika kuwawezesha kuzalisha kazi zao kwa viwango na ubora stahiki kulingana na mahitaji ya soko.
Akizungumza kwenye kikao cha wadau wa filamu, mkoani hapa jana, Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Dkt. Kiagho Kilonzo, alisema kasi ya mafunzo ya muda mfupi yaani ‘masterclases’ inaendelea katika kuwawezesha wasanii watasnia hiyo kuboresha kazi zao.
“Mpaka sasa mafunzo yamefanyika kwenye mikoa tisa nchini chini ya ufadhili wa serikali, ya namna ya kuboresha uzalishaji wa filamu kupitia mafunzo ya muda mfupi,” alisema Kilonzo
Aidha, alisema juhudi za Serikali za kuzunguka maeneo mbalimbali duniani kwa lengo la kutafuta wataalamu mbalimbali wa kuendesha programu za mafunzo zimeendelea kutoa matumaini, ambapo mpaka sasa tayari wamefanikiwa kuwapata, na muda wowote wasanii watatangaziwa utaratibu wa mafunzo hayo ilikupata fursa ya kushiriki.
Kilonzo ambaye alikuwa akizungumza kabla ya kumkaribisha NaibuWaziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza kuzungumza, alisema juhudi zilizopo kwa sasa wanaendelea kutafuta soko la uhakika la filamu za kitanzania ili kuwapa wazalishaji na wadau wote hamasa ya kufaidi matunda ya kazi zao.
“Mpaka hivi nina vyo zungumza tayari wanigeria wamejitokeza wanahitaji hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu wawe na ‘story’ kati ya hamsini hadi mia moja za kitanzania, hivyo na wahimiza wasanii changamkieni fursa hiyo anzeni kutengeneza hadithi za kiafrika zinazoweza kuuzika nje ya Tanzania,” alisema
Mbali na hilo, wadau wa filamu kutoka taifa la Namibia nao pia wameonyesha utayari wa kufanya ‘uzalishishirikishi’ kwa kuungana pamojana wasanii wa filamu wa kitanzania kutengeneza kazi zitakazo uzwa nchi zote mbili, taarifa kamili kuhusu mchakato huo unatarajiwa kutangazwa kuanzia mapema mwezi Machi mwaka huu.
Aidha, Kilonzo alisema ilikuboresha kipato na kukabiliana na changamoto ya ajira kwenye tasnia ya filamu nchini, serikali ikiwa ndani ya taifa la Uingereza, ilikutana na makampuni 15 ambayo yalionyesha nia ya kuja kuwekeza nchini, na yatakapowasili kulingana na kanunina taratibu za Tanzania basi wawekezaji hao wa filamu watalazimika kuchukua sehemu kubwa ya nguvukazi ya ndani ya watanzania
Sambambana hilo, alisema wadau wa Shirikisho la Filamu kutoka India ‘Bollywood’ nao mapema mwezi June watawasili nchini, ambao tayari wamehitaji kupata wasanii wa kitanzania wapatao 100, ilikushirikiana kwa pamoja katika kukamilisha azma yao.
Hata hivyo, mchakato wa bodi uliopo kwa kushirikiana nawadau, nikuanza kushindanisha kazi mbalimbali za Sanaa ya filamu kupitia kumbi za maonyesho lengo likiwa ni kupata filamu moja bora ambayo hatimaye itaingia kwenye soko la kimataifa, na sehemu ya fedha ya viingilio atapewa mzalishaji wa kazi husika.
Akizungumzia kuhusu hatua ya upatikanaji wa Katiba ya Shirikisho unaoendelea, Kilonzo alisema serikali imeweza kudhamini kikamilifu hatua kwa hatua mchakato huo kwa mafanikio, huku hatua iliyobaki kwa sasa ni ile ya Mkutano Mkuu wa Shirikisho ambao unatarajiwa kukaa kwa mara ya mwisho ifikapo Januari 28 mwaka huu.
“Hatua zilizofikiwa mpaka sasa ni kwamba serikali iliunda timu kupitia ile katiba na kuizungusha nchi nzima, na ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vingine vya habari ili kutoa fursa ya wadau kutoa maoni yao kutakaiweje, na mpaka sasa mkutano mkuu umeshakaa vikao viwili huku kile cha mwisho kikisubiriwa,” alisema
Kwa upande wake, Shonza pamoja na mambo mengine, aliwataka wasanii wafilamu nchini kubadilika na kuacha kufanya kazi kwa mazoea, ili kwenda sanjari na mahitaji ya walaji kwa kuzingatia vigezo vyote muhimu, huku akirudia kusisitiza suala la ubora mara kwa mara.
Alisema barani Africa Tanzania inashika nafasi ya pili kwa uzalishaji wa filamu nyingi,ikitanguliwa na Nigeria, huku akiwataka wasanii kujipanga kwanza na hatimaye kutoa angalau filamu moja tu kwa mwaka itakayokuwa na ubora na hatimaye kuweza kumtambulisha vizuri zaidi msanii kwenye soko.
Shonza aliwataka wasanii kote nchini kuondokana na mfumo wa kutengeneza movie na kuweka kwenye DVD huku akisema ni rahisi kuibiwa, badala yake msanii aanze kwanza kwa uzinduzi kwenye kumbi za sinema kabla ya kutupia kwenye mtandao ili msanii kujihakikishia idadi kubwa ya watazamaji na soko la uhakika.
“Nataka niwahakikishieni filamu za watanzania zinapendwas ana, na wala tatizo sio masoko…soko lenyewe la Afrika Mashariki bado hatujalimaliza, kinachotakiwa kwa sasa ni kuboresha filamu zetu ziwe katika ubora,” alisema na kuongeza:
“Kama tatizo ni fedha jiongezeni jiungeni kwenye vikundi, nendeni halmashauri kuna mikopo ya vijana, wanawake na wenyeulemavu, ipokisheria pale asilimia 10 imetengwa, kachukueni mfanye ujasiriamali na faida mtakayo ipata boreshenis anaa yenu”.