UTEUZI: Rais John Magufuli amemteua, George Simbachawene kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani akichukua nafasi ya Kangi Lugola ambaye nafasi yake imetenguliwa.
Pia amemteua Musa Azzan Zungu kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira akichukua nafasi ya George Simbachawene aliyeteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi.