Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Angelina Mabula akiwa ameongozana na Meneja wa Mawasiliano wa Shirika la Nyumba na Mkuu wa wilaya ya Mpanda Lilian Matinga katika mradi wa nyumba za kuishi Ilembo
Jengo la uwekezaji la Shirika la Nyumba lililopo katika Manispaa ya Mpanda
***************************
Na Mwandishi wetu, Katavi
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi mheshimiwa Angelina Mabula amelitaka Shirika la Nyumba nchini kutekeleza miradi waliyonayo kwa wakatai ili kuendelea kujenga imani kati yao halmashauri na taasisi wanazofanya nazo kazi
Mheshimiwa Mabula ametoa ushauri huo wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Katavi ambapo pia amepata fursa ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Shirika la Nyumba
Aliwataka kukamilisha miradi kwa kujibu wa mikataba waliyowekeana na halmashauri.
“kama mlikubaliana vizuri tena kwa amani kwanini nanyi msifanye kazi na kumaliza kwa wakati msisubiri wateja waanze kulalamika” alisema Mabula
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na viongozi wa shirika hilo; wamesema licha ya kukabiliwa na changamoto ya kuwa na wateja wachache wangali wanatekeleza jumla ya miradi 17 mkoani katavi
Kaimu Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Katavi Masumbuko Majaliwa ametaja miradi waliyonayo kuwa ni pamoja na jengo la Ghorofa tano lililopo katika Manispaa ya Mpanda ambalo linapangishwa vyumba vya ofisi na maeneo ya biashara
Kwa upande wake Meneja Mawasiliano wa Shirika la Nyumba Muungano Sabuya amesema mbali na kuwa na miradi hiyo pia wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa wateja wa kutosha
Aidha baadhi ya wanufaika miradi inayotekelezwa na shirika la nyumba ni pamoja wakala wa huduma za misitu wilaya ya mlele; ambao wamesema mradi huo ukikamilika wataondokana na changamoto ya ufinyu wa ofisi
“Kwa kazi tulizonazo ofisi hii ikikamilika tutaweza kuwa na vyumba vya kutosha kuwawezesha maafisa wetu kufanya kazi vizuri, tuna misitu mitano tunayosimamia” alisema Fredrick Kasilema ambaye ni kaimu Meneja Wakala wa Misitu Mlele