******************************
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Seriakli imezidi kubana mianya ya wiza wa mapato ya ndani katika Mamlaka za Serikali za mitaa kwa kukabidhi mashine za kukusanyia mapato kwa njia ya kielektroniki 7227 zenye mfumo madhubuti wa kudhibiti wadanganyifu kucheza na mashine hizo.
Zoezi la kukabidhi mashine hizo zenye muonekano unaofanana na utambulisho wa Serikali wakati zinapowashwa na kuzimwa limefanywa na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Mhe. Seleman Jafo Jijini Dodoma mapema leo kwa Wakurugenzi waHalmashauri zote 185.
Akikabidhi mashine hizo Jafo aesema kuna watu walikua wanaendelea na ujanja wa kudukua mifumo ya mashine zilizokuwa zinatumika kukusanya mapato ikiwemo kubadili tarehe na na kuzima internet ili fedha hizo zisisomeke kwenye mfumo wa Serikali.
Aliongeza kuwa mashine za awali zilikuwa rahisi katika kubadiri baadhi ya taarifa ndiyo maana wameamua kuja na mfumo mwingine unaokwenda kuzuia kabisa wizi huo.
“Sasa mwisho wa udanganyifu wa naman hii umekwisha kwanza mashine hizi tumeziagiza wenyewe na kuweka mfumo tunaotumia sisi na hauruhusu kubadilisha tarehe wala kuzima internet hivyo chochote kitakachotokea
kwenye mashine hiyo kitaripotiwa na kubainika mara moja” alisema Jafo.
Hata hivyo, Jafo alisema licha ya baadhi ya halmashauri kuwa na makusanyo makubwa, lakini anapata kichefuchefu kuona wanashindwa kujenga hata na matundu ya vyoo vya walimu katika maeneo yao.
“Tunakwenda kuziba mapengo ya wizi, lakini kuna watu wanakatisha tamaa kwani hadi mwishoni wa desemba mwaka jana, hawakuwa wamefikia hata asilimia 20 ya malengo ya makusanyo wakati wengine walikuwa zaidi ya asilimia 50,” alisema Jafo.
Akizungumzia kuhusu mashine hizo, alisema zinakwenda kuongeza idadi kwani awali kulikuwa na mashine 10,100 katika halmashauri zote nchini hivyo kwa sasa kutakuwa na mashine 17,327 ambazo zitapelekea halmashauri kuwa na uwezo wa kukusanyo juu zaidi.