********************************
Na Mwandishi wetu Mihambwe
Afisa Tarafa Mihambwe, Emmanuel Shilatu leo amefanya ziara kukagua ujenzi wa miradi ya kimaendeleo inayofanyika ndani ya Tarafa ya Mihambwe na kuagiza miradi hiyo ikamilike kwa wakati kwa kuzingatia ubora unaolingana na thamani ya fedha.
Gavana Shilatu amepita kwenye kata na vijiji mbalimbali ambapo ametembelea ujenzi wa miradi ya Madarasa, Maabara na vyoo katika shule zilizopo ndani ya Tarafa ya Mihambwe na kukuta mafundi wakiendelea na ujenzi.
Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo, Gavana Shilatu amesisitiza vyoo vijengwe kwa kuzingatia mahitaji ya Watu maalum; Madarasa yakamilike pamoja na Madawati yake na Maabara yazingatie viwango na ubora stahiki.
“Nimezunguka kujionea ujenzi wa miradi ya kimaendeleo, nimetoa maelekezo miradi ikamilike kwa wakati kwa kuzingatia ubora unaolingana na thamani ya fedha. Nimesisitiza ukamilifu kwa wakati ili matumizi yake yaanze mara moja.” Alisema Gavana Shilatu.
Gavana Shilatu aliongezea, “Ujenzi wa vyoo uzingatie mahitaji maalum ya Walemavu na Mabinti; Madarasa yakamilike pamoja na Madawati yake; na Maabara zizingatie ubora stahiki.”.
Shule zilizotembelea leo na Gavana Shilatu ni Shule ya Sekondari ya Mweminaki, Shule ya Sekondari ya Mihambwe, Shule ya Sekondari ya Mkoreha, Shule ya msingi ya Mihambwe, Shule ya Msingi ya Miuta, Shule ya Msingi ya Ngongo na Shule ya Msingi ya Ruvuma.
Katika ziara hiyo Gavana Shilatu aliambatana na Watendaji Kata, Watendaji Vijiji, Maafisa Elimu Kata, Kamati za ujenzi za miradi husika pamoja uongozi wa shule husika.