Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mhandisi Pascas Muragiri akihamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo.
Msemaji wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani hapa, Ahmed Athman maarufu “Kaburu”akizungumzia kukamilika kwa ukarabati wa uwanja huo.
Maandalizi ya mechi kati ya yanga na Singida united yakiendelea.
Na MwandishiWetu, Singida
MAANDALIZI ya Mechi ya Ligi Kuu Bara, Yanga dhidi ya wenyeji wao Singida United inayotarajiwa kutimua vumbi ndani ya uwanja wa“Liti” mkoani hapa kesho (Namfua Stadium) yamekamilika, huku mashabiki na wenyeji wa mkoa huo na viunga vyake wakiombwa kujitokeza kwa wingi ilikutoa hamasa ya ushindi kwa timu yao ya Singida United
Timu ya Yanga tayari imeshawasil imkoani hapa tangu jana usiku tayari kukabiliana na Singida United hiyo kesho, mchezo utakao chezwa kuanzia majira ya saa 10 jioni, hukuhisia, macho na masikio ya mashabiki wengi vikielekezwa zaidi kwa timu ya Yanga kujua ‘itatokaje’ kutokana na kutofanya vizuri sana kwenye mechi zake za hivi karibuni
Msemaji wa Singida United, Cales Katemana amesema kwa upande wao wamejiandaa vizuri, timu ipotimamu kabisa katika kuhakikisha wanajinyakulia pointi tatu muhimu kuwawezesha kusongambele zaidi kwenye michuano hiyo.
“Mchezo huu dhidi ya Yanga kwetu tunahesabu ni mchezo wakawaida, natunakwenda kucheza na moja ya timu ya ligi kuu kama zilivyo nyingine. Kikubwa watanzania waeleweSingida United ipo vizuri tena vizuri sana, na watarajie ushindi mnono dhidi ya Yanga,” alisema Katemana
Katemana alisema kamati wameridhishwa na maboresho ya uwanja yanayoendelea kufanyika kwa kasi, nahasa ‘Pitch’ yenyewe ambayo kwa sasa ipo katika ubora na viwango vinavyotakiwa kwaajili ya mchezo huo.
Akizungumzia mchezo huo, Msemajiwa Yanga, Hasan Bumbuli, alisema mechi dhid iya Singida United ni ngumu kwa upande wao, anafahamu timu hiyo imefanya usajili mkubwa hivi karibuni lakini hata hivyo Yanga imejipanga kuhakikisha haipotezi tena mchezo wowote kuanzia hiyo kesho.
“Nawaomba mashabiki wa Yanga mjitokeze kwa wingi kuishangilia timu yetu, tunafahamu kwanamna moja au nyingine tumewa-disapoint kutokana na matokeo yasiyoridhisha kwenye mech izilizotangulia lakini ni wahakikishie kwa sasa timu ipo vizuri…natarajieni matokeo mazuri kwenye mchezo wa kesho,” alisema Bumbuli
Kwa upande wake, Msemajiwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani hapa, Ahmed Athman maarufu “Kaburu”ambao ndio wamiliki wa uwanja huo, alisema chama hicho kwa sasa kinaendelea kufanya maboresho makubwa kwenye eneo l ote la uwanja wa “Liti” kuhakikisha unarudi katika viwango na ubora kulingana na matakwatarajiwa.
“Ibaraya 161 inasema CCM itaimarisha viwanja vyake vyote ilikuwawezesha vijana kupata ajira, kama unavyotazama hali ya uwanja kwa sasa nyasi zipo kwenye mpangilio na viwango huku maboresho mengine yakiwa yanaendelea,” alisema Athman wakati akinukuu sehemu y aIlani ya CCM
Mpaka muda huu, Yanga ipo kwenye nafasi ya 7, ikiwa na alama 25, huku wenyeji wao Singida United wakiwa kwenye nafasi ya 19 n aalama 10 kwenye msimamo wa Ligi Kuu inayoendelea