Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ,akiongoza kikao na wadau wa tasnia ya Pamba ili kufanya mapitio ya ununuzi na uuzaji kwa msimu uliopita na kujiandaa na msimu ujao jijini Dodoma kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa CRDB Abdumajid Isekela
Sehemu ya wadau wa tasnia ya Pamba wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe (hayupo pichani) kikao hicho kimefanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ,akizungumza na waandishi wa habari (ghawapo pichani ) mara baada ya kufanya mazungumzo na wadau wa tasnia ya Pamba ili kufanya mapitio ya ununuzi na uuzaji kwa msimu uliopita na kujiandaa na msimu ujao jijini Dodoma
Mkurugenzi Mkuu wa CRDB Abdumajid Isekela,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kikao cha Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe na wadau wa tasnia ya Pamba ili kufanya mapitio ya ununuzi na uuzaji kwa msimu uliopita na kujiandaa na msimu ujao kilichofanyika jijini Dodoma.
Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog
………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amefanya mazungumzo na wadau wa tasnia ya pamba ili kufanya mapitio ya ununuzi na uuzaji kwa msimu uliopita na kujiandaa kwa msimu ujao.
Aidha kikao hicho kimehudhuriwa na Taasisi za fedha,bodi ya pambaa pamoja na wanunuzi wa pamba katika kupata mwenendo mzima wa pamba kwa msimu uliopita.
Mhe Bashe amesema Serikali ilitoa maelekezo katika msimu wa pamba kuwa pamba yote inunuliwe na sekta binafsi iwapatie fedha kwa ajili ya kununua na kulikuwa na mapitio kujua hali ikoje na wameuza kiasi gani nje mpaka sasa na kwa takwimu za haraka ni kwamba karibu asilimia 80 imeshauzwa nje huku msimu mpya umeshaanza .
“ Wakulima safari hii waligaiwa mbegu kwa mkopo wote kwa hiyo tulikuwa tunajaribu kuangalia kwa ajili ya majadiliano ya awali kufanya mapitio ya msimu uliopita vilevile kujiandaa kwa msimu ujao”amesisitiza Mhe.Bashe
Hata hivyo ameongeza kuwa safari hii pamba ilinunuliwa chini ya usimamizi wa serikali na sekta ya fedha ambapo kulikuwa na makubaliano kati ya serikali na wanunuzi,msimamizi ambaye ni Benki kuu .
‘’Hivyo kikao hiki ni kwa ajili ya kupitia kwa ufupi, kuangalia na kupeana muda mpaka wiki ijayo kila mnunuzi alete taarifa ameuza kwa shilingi ngapi,gharama zake ni shilingi ngapi ili waone ni namna gani ahadi za Serikali zinaenda kwenye utekelezaji’’ Amesema Mhe.Bashe
Aidha amesema kuwa jambo jingine muhimu katika majadiliano ni kukubaliana kwamba msimu unaokuja malipo yote yatakuwa kupitiaa benki na hakutakuwa na mambo yakulipana cash.
“Changamoto ambayo tunayo kwa sasa ni kwamba wanunuzi wanadaiwa fedha za AMCOS,lakini AMCOS zimetumia fedha za kuwalipa malipo ya wakulima kwa ajili ya kulipia shughuli za uendeshaji kwa hiyo unakuta kwenye baadhi ya maeneo kuna wakulima wachache wanadai “Ameongeza kusema
Hata hivyo Bashe amesema wanakusanya hizo takwimu kupitia bodi halafu wakishamaliza hii ripoti kupitia kikosi kazi ambacho kitakuwa kinaongozwa na Mwenyekiti wa Mabenki kwamba kabla ya tarehe 31 januari kuwe tayari na taarifa rasmi .
Aidha amewaomba wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kutochukua hatua za kutumia nguvu katika kukusanya sec kutoka kwa wafanya biashara kwa sababu kutakuwa na kikao ambacho kitatoa maamuzi ya pamoja ya malipo ya shilingi 33 kwa ajili ya AMCOS.
Pia amesema jumla ya kampuni ambazo zimenunua pamba mwaka huu ni 23 kutoka kwa wakulima jumla ya tani 350,000 ambazo zimenunuliwa kiujumla ambazo ni kilo milioni 350 na wafanyabiashara wa Tanzania wengi wamebaki na kiwango kisichozidi asilimia kumi mpaka sasa.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa CRDB Abdumajid Isekela amesema kuwa amefurahishwa na ushirikianao ambao wizara inafanya kati ya taasisi za fedha na wanunuzi wa pamba na kusema kuwa mabenki yalishiriki kwa kina sana msimu uliopita kwenye kukopesha ambapo wamiliki wa mabenki wameshiriki katika kikao hiki ili kuangalia mwenendo wa ununuzi wa pamba ulivyokwenda.