Beki wa Arsenal, Hector Bellerin (kulia) akishangilia na Granit Xhaka baada ya kuifungia timu hiyo bao la kusawazisha zikiwa zimesalia dakika tatu katika sare ya 2-2 na wenyeji, Chelsea usiku wa jana kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London. Bao lingine la Arsenal iliyomaliza pungufu baada ya beki wake wa kati, David Luiz kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kumchezea rafu Tammy Abraham kwenye boksi lilifungwa na Gabriel Martinelli dakika ya 63, wakati ya Chelsea yalifungwa na Jorginho kwa penalti dakika ya 28 na Cesar Azpilicueta dakika ya 84 PICHA ZAIDI SOMA HAPA
ARSENAL WALIOCHEZA PUNGUFU WAICHOMOLEA CHELSEA 2-2 DARAJANI
By Alex Sonna
January 22, 2020 | 11:30 am

Related Stories
View all
Michezo
2 days ago
YANGA YAIONDOA SIMBA SC KILELENI LIGI KUU TANZANIA BARA
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Young Africans SC, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa…
Michezo
3 days ago
SIMBA SC YAREJESHA MATUMAINI YA UBINGWA LIGI KUU NBC
Wekundu wa Msimbazi Simba SC imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara…
