Home Mchanganyiko PICHA ZA WATUHUMIWA WA UTUPAJI TAKA NGUMU OVYO

PICHA ZA WATUHUMIWA WA UTUPAJI TAKA NGUMU OVYO

0

Baadhi ya watuhumiwa  wa  kosa la utupaji taka ovyo, wakiingia  katika gari la Mahakama Inayotembea leo, wakati gari  hilo likiwa ngazi ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine  maafrufu ‘Mahakama ya Jiji’ kwa ajili ya kusikiliza mashauri yao kwenye  viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bi. Sophia  Mjema (wa pili kushoto) akiwa katika gari la Mahakama Inayotembea leo kwa ajili  ya kusikiliza mashauri ya watuhumiwa wa utupaji wa taka ngumu ovyo baada ya kuvunja  Sheria ya Mazingira namba mbili ya Mwaka 2004, pamoja na sheria ndogondogo  za jiji , wakati gari  hilo likiwa ngazi ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine maarufu  ‘Mahakama ya Jiji’ kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala,  Bi. Sophia Mjema (kushoto) akizungumza jambo  leo na  Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Mhe. Martha Mpaze ,wakati gari la Mahakama Inayotembea,  likiwa ngazi ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine  maarufu ‘Mahakama ya Jiji’.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala,  Bi. Sophia Mjema (kushoto) akizungumza jambo  leo na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Bw. Omary Kumbilamoto wakati gari la Mahakama Inayotembea,  likiwa ngazi ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine  maarufu ‘Mahakama ya Jiji’.

(Picha na Magreth Kinabo- Mahakama)