Baadhi ya watuhumiwa wa kosa la utupaji taka ovyo, wakiingia katika gari la Mahakama Inayotembea leo, wakati gari hilo likiwa ngazi ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine maafrufu ‘Mahakama ya Jiji’ kwa ajili ya kusikiliza mashauri yao kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bi. Sophia Mjema (wa pili kushoto) akiwa katika gari la Mahakama Inayotembea leo kwa ajili ya kusikiliza mashauri ya watuhumiwa wa utupaji wa taka ngumu ovyo baada ya kuvunja Sheria ya Mazingira namba mbili ya Mwaka 2004, pamoja na sheria ndogondogo za jiji , wakati gari hilo likiwa ngazi ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine maarufu ‘Mahakama ya Jiji’ kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bi. Sophia Mjema (kushoto) akizungumza jambo leo na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Mhe. Martha Mpaze ,wakati gari la Mahakama Inayotembea, likiwa ngazi ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine maarufu ‘Mahakama ya Jiji’.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bi. Sophia Mjema (kushoto) akizungumza jambo leo na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Bw. Omary Kumbilamoto wakati gari la Mahakama Inayotembea, likiwa ngazi ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine maarufu ‘Mahakama ya Jiji’.
(Picha na Magreth Kinabo- Mahakama)