******************************
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mhe. Regine Hess kwenye ofisi za wizara jijini Dodoma.
Katika Mazungumzo yao Waziri Ummy Mwalimu aliishukuru nchi hiyo kwa mashirikiano yao katika sekta ya afya hususan afya ya msingi kupitia shirika la GIZ na KFW toka mwaka 2003.
Naye Balozi Mhe.Regine amesema nchi yao itaendelea kuisaidia Tanzania katika kuwajengea uwezo watumishi wa afya na katika maeneo mengine katika nyanja za afya.
Tanzania na Ujerumani zimeanza mashirikiano toka mwaka 1961.