Baadhi ya Wadau wa maswala ya Biashara waliohudhuria katika Mkutano wa Taasisi ya Kufanya Utafiti wa Uchumi na Sera (REPOA)kuhusiana na Mpango wa kuhimili Ushindani wa Kibiashara hafla ilofanyika Hoteli Verde Maruhubi Zanzibar.
Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi Amina Salum Ali(Katikati)akiwa katika picha ya pamoja na Wadau na Viongozi Katika Mkutano wa Taasisi ya Kufanya Utafiti wa Uchumi na Sera (REPOA)kuhusiana na Mpango wa kuhimili Ushindani wa Kibiashara hafla ilofanyika Hoteli Verde Maruhubi Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya kufanya Utafiti wa Uchumi na Sera (REPOA) Dkt,Donald Mmari akitoa hotuba ya makaribisho katika Mkutano wa Taasisi ya Kufanya Utafiti wa Uchumi na Sera (REPOA)kuhusiana na Mpango wa kuhimili Ushindani wa Kibiashara hafla ilofanyika Hoteli Verde Maruhubi Zanzibar.
Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi Amina Salum Ali akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano wa Taasisi ya Kufanya Utafiti wa Uchumi na Sera (REPOA)kuhusiana na Mpango wa kuhimili Ushindani wa Kibiashara hafla ilofanyika Hoteli Verde Maruhubi Zanzibar.
Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi Amina Salum Ali akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa Taasisi ya Kufanya Utafiti wa Uchumi na Sera (REPOA)kuhusiana na Mpango wa kuhimili Ushindani wa Kibiashara hafla ilofanyika Hoteli Verde Maruhubi Zanzibar.
Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar 20/01/2020
Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi Amina Salum Ali amesema ushindani wa bidhaa nchini unahitaji mpangilio maalum unaotokana na sera, sheria pamoja na soko la uuzwaji wa bidhaa hizo .
Hayo ameyasema wakati akifungua Mkutano wa Wajasiriamali kuhusiano na Mpango wa kuhimili ushindani wa kibiashara nchini huko katika Hoteli ya Verde Maruhubi .
Alisema ushindani wa biashara unahitaji mpangilio kwa kutoa mafunzo ya uzalishaji wa bidhaa kwa wajasiriamali ili kuweza kufuata maadili ya wataalamu kwa kukuza uzalishaji na kuongeza kipato kwa wafanyabiashara wadogo wadogo.
Alisema kuwa wajasiriamali wa bidhaa ya mwani wameweza kupatiwa mafunzo ya mwani wa aina mpya ambayo unauwezo wa kutoa mbegu ya mwani kwa wingi hadi mashamba kuimarika na kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa hiyo .
Aidha alisema Wajasiriamali waliopata mafunzo kwa upande wa Pemba ni katika Kijiji cha Makangale ,Tumbe ,Chokocho pamoja na Kusini, Kaskazini na Magharibi kwa Upande wa Unguja .
Alifahamisha kuwa changamoto zilizopo kwa wasiriamali hao ni ukosefu wa baadhi ya vifaa vya kufanyia kazi pamoja na boti ya uokozi pia wanahitaji mafunzo ya uokoaji na upigaji mbizi .
Alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar tayari imeshatiliana Mkataba katika Kampuni mbili tofauti pamoja na Utayarishaji wa ujenzi wa kiwanda cha mwani.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa Dr.Donald Mmari amesema wamekuwa wakishughulikia sera ya masoko ya ndani na ya nje ya bidhaa mbali mbali ikiwemo bidhaa za mbogamboga ngozi pamoja na zao la mpunga kwa lengo la kuimarisha bidhaa hizo ili ziweze kuingia katika ushindani wa kIbiashara .
Alifahamisha kuwa kwa upande wa bidhaa ya mwani huwasaidia kipato kwa wakulima wa mwani kutokana na kukuwa kwa uzalishaji wa bidhaa hiyo na kuweza kumiliki soko la ushindani
Alisema sera ya viwanda ina lengo la kukuza uzalishaji wa bidhaa kwa kukidhi mahitaji ya masoko pamoja na kuweza kuingia katika soko la ushindani .