***********************************
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limefanikiwa kuwaua majambazi wa watatu na kufanikawa kukamata silaha moja aina ya bastola iliyofutwa namba pamoja na magazine iliyokuwa na risasi moja.
Mnamo 19.01.2020 majira ya 7:30 mchana huko maeneo ya Magomeni katika ufuatiliaji wa wahalifu, ghafla Askari Polisi waliokuwa katika doria walishambuliwa kwa risasi na majambazi ambao walihisi kuwa wanafuatiliwa na ndipo askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi
majambazi watatu kwa risasi na wakati wanakimbizwa katika ya Hospitali Mhimbili kwaajili ya matibabu walifariki dunia.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa majambazi hao wamekuwa wakifanya matukio mbalimbali ya kihalifu maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salama
na mikoa ya jirani.
Jeshi la Polisi linaendelea na msako mkali wa wahalifu wote wanaofanya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dsm, wananchi waendelee kutupa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.