Home Mchanganyiko NAIBU WAZIRI MANYANYA AZINDUA TEKNOLOJIA MPYA YA KUCHAKATA ZABIBU,ILIYOBUNIWA NA TEMDO NA...

NAIBU WAZIRI MANYANYA AZINDUA TEKNOLOJIA MPYA YA KUCHAKATA ZABIBU,ILIYOBUNIWA NA TEMDO NA SIDO

0

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stellah Manyanya,akisalimiana na Meneja wa Taasisi ya Ubunifu na uhandisi Mitambo, (TEMDO), Mhandisi Elexisander Komba alipowasili katika alipokwenda kuzindua Technolojia mpya ya mashine ya kukamua mchuzi wa Zao la Zabibu katika kiwanda kidogo Cha WENDECE kilichopo Kata ya Hombolo Bwawani, Wilaya ya Dodoma.

Meneja wa SIDO Mkoa wa Dodoma, Sempeho Manongi,akizungumza na wakulima na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa Technolojia mpya ya mashine ya kukamua mchuzi wa Zao la Zabibu katika kiwanda kidogo Cha WENDECE kilichopo Kata ya Hombolo Bwawani, Wilaya ya Dodoma kulia kwake ni mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stellah Manyanya.

Meneja wa Taasisi ya Ubunifu na uhandisi Mitambo, (TEMDO), Mhandisi Elexisander Komba,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Technolojia mpya ya mashine ya kukamua mchuzi wa Zao la Zabibu katika kiwanda kidogo Cha WENDECE kilichopo Kata ya Hombolo Bwawani, Wilaya ya Dodoma kushoto kwake ni mgeni rasmi ambaye ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stellah Manyanya.

Mmiliki wa  Kiwanda Cha WENDECE Evarist Maganga,akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stellah Manyanya kabla ya kuzindua Technolojia mpya ya mashine ya kukamua mchuzi wa Zao la Zabibu katika kiwanda kidogo Cha WENDECE kilichopo Kata ya Hombolo Bwawani, Wilaya ya Dodoma.

Diwani wa kata ya Bwawani Ased Ndajilo akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stellah Manyanya ambaye alizindua Technolojia mpya ya mashine ya kukamua mchuzi wa Zao la Zabibu katika kiwanda kidogo Cha WENDECE kilichopo Kata ya Hombolo Bwawani, Wilaya ya Dodoma.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stellah Manyanya,akizungumza na wakulima wakati wa uzinduzi wa  Technolojia mpya ya mashine ya kukamua mchuzi wa Zao la Zabibu katika kiwanda kidogo Cha WENDECE kilichopo Kata ya Hombolo Bwawani, Wilaya ya Dodoma.

Sehemu ya wakulima wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stellah Manyanya wakati wa uzinduzi wa  Technolojia mpya ya mashine ya kukamua mchuzi wa Zao la Zabibu katika kiwanda kidogo Cha WENDECE kilichopo Kata ya Hombolo Bwawani, Wilaya ya Dodoma.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stellah Manyanya,akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa  Technolojia mpya ya mashine ya kukamua mchuzi wa Zao la Zabibu katika kiwanda kidogo Cha WENDECE kilichopo Kata ya Hombolo Bwawani, Wilaya ya Dodoma.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stellah Manyanya,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  Technolojia mpya ya mashine ya kukamua mchuzi wa Zao la Zabibu katika kiwanda kidogo Cha WENDECE kilichopo Kata ya Hombolo Bwawani, Wilaya ya Dodoma.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stellah Manyanya,akiw na viongozi wakifurahia jambo mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa  Technolojia mpya ya mashine ya kukamua mchuzi wa Zao la Zabibu katika kiwanda kidogo Cha WENDECE kilichopo Kata ya Hombolo Bwawani, Wilaya ya Dodoma.

Muonekano wa mashine ya kuchakata mchuzi wa Zabibu.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stellah Manyanya,akitoa maelezo mara baada ya kuzinduzi wa  Technolojia mpya ya mashine ya kukamua mchuzi wa Zao la Zabibu katika kiwanda kidogo Cha WENDECE kilichopo Kata ya Hombolo Bwawani, Wilaya ya Dodoma.

Mmiliki wa  Kiwanda Cha WENDECE Evarist Maganga,akimuonesha Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stellah Manyanya,jinsi mashine inavyokamua  mchuzi wa Zao la Zabibu katika kiwanda kidogo Cha WENDECE kilichopo Kata ya Hombolo Bwawani, Wilaya ya Dodoma.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stellah Manyanya,akiangalia  mashine zinazokamua  mchuzi wa Zao la Zabibu katika kiwanda kidogo Cha WENDECE kilichopo Kata ya Hombolo Bwawani, Wilaya ya Dodoma.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stellah Manyanya,akiangalia waini zinazotengenezwa  katika kiwanda kidogo Cha WENDECE kilichopo Kata ya Hombolo Bwawani, Wilaya ya Dodoma.

PICHA NA ALEX SONNA-FULLSHANGWE BLOG

……………………

Na.Alex Sonna,Hombolo

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stellah Manyanya, amesema endapo taasisi zinazofanya utafiti na  zinazobuni na kutekeleza technolojia rahisi hapa nchini zitawezeshwa kifedha basi tutafikia lengo la kuwa na viwanda na kufikia uchumi wa Viwanda.

Mhandisi Stellah Manyanya ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akizinduaTtechnolojia mpya ya mashine ya kukamua mchuzi wa Zao la Zabibu katika kiwanda kidogo Cha WENDECE kilichopo Kata ya Hombolo Bwawani, Wilaya ya Dodoma, Technolojia iliyobuniwa na SIDO kwa kushirikiana na TEMDO.

Amesema Kuna haja ya kuziwezesha taasisi Kama SIDO, TEMDO, CAMATEC na zinginezo, kwani kwa muda mrefu taasisi hizo zilikuwepo lakini hazikuweza kutunufaisha, lakini  tangu zimewezeshwa kifedha tayari matokeo yameanza kuonekana.

“Taasisi hizi zilikuwa hazitengewi fedha lakini baada ya kuanza kiziwezesha matokeo tumeanza kuyaona, tena tumewapa shilingi milioni Mia tatu(300) na tayari matokeo tunayaona tena kwa mda mfupi” amesema Mhandisi Manyanya.

Amesema kumbe uwezekano wa kutekeleza teknolojia rahisi zenye uwezo wa kuwanufaisha wajasiliamali na wakaachana na changamoto hizo kikubwa ni kiziwezesha kifedha tu taasisi hizo.

Aidha amewahimiza watanzania kuthamini vitu vinavyotengenezwa hapa nchini, ikiwamo kuthamini viwanda vidogo kwa sababu vinasaidia kutoa ajira kwa watanzania, huku akiitaka SIDO kuhakikisha inasimamia Wenye viwanda vidogo kuhakikisha wanapata mikopo kutoka Benki ya kilimo, ili kuwaongezea nguvu wajasiliamali hawa wanaothubutu.

“Hii Benki ya Kilimo inakopesha akina nani? inakopesha wakubwawakubwa tu, nataka SIDO muwasiliane na Benki ili iweze kuwakopesha hata hawa pia ambao tayari wamethubutu na wameonesha mwanga” amesema.

Nae Meneja wa Taasisi ya Ubunifu na uhandisi Mitambo, (TEMDO), Mhandisi Elexisander Komba, amesema kazi yao ni kubuni na kuendeleza Technolojia kwa ajili ya wajasiliamali wazalishaji, Kisha kupeleka kwa SIDO ili ziweze kuwafikia walengwa.

“Sisi kazi yetu ni kubuni na kutengeneza mashine na Mitambo mingine na kuwapelekea wahusika ili ziweze kuwafikia wahusika, Kama tulivyofanya katika hii mashine” amesema Komba.

Kwa upande wake  Meneja wa SIDO Mkoa wa Dodoma, Sempeho Manongi, amesema teknolojia hiyo itaweza kurahisisha uchakataji wa Zao la Zabibu kwa mwanzo walikuwa wakihangaika kwa kutokuwa na teknolojia ya kuwarahisishia kazi.

Kwa upande Mmiliki wa  Kiwanda Cha WENDECE Evarist Maganga,amesema kuwa  teknolojia hiyo imeanza kufanya kazi katika kiwanda hicho pia  mashine  imekuwa mkombozi  wao na wakulima kwa ujumla kwani mwanzo mazao mengi yalikuwa yakiozea mashambani.

”Lakini baada ya kuja kwa teknolojia hiyo Sasa wakulima wanauhakika wa kuuza mazao yao na wao kuchakata mazao hayo kwa wakati, pia ameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa jinsi inavyojitahidi kuwawezesha”amesisitiza