Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akisalimiana na wanawake wa vikundi vya DARE na Ulonge vinavyojishughulisha na ujenzi wa barabara na madaraja madogo wilayani Ludewa mkoai Njombe katika ziara yake mkoani humo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifurahia mara baada ya kupokea zawadi ya jogoo kutoka kwa kikundi cha vikundi vya DARE na Ulonge vinavyojishughulisha na ujenzi wa barabra na madaraja madogo wilayani Ludewa mkoani Njombe katika ziara yake mkoani humo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile( mwenye shati la njano na kijani) akiwa katika picha ya pamoja vikundi vya DARE na Ulonge vinavyojishughulisha na ujenzi wa barabra na madaraja madogo wilayani Ludewa mkoani Njombe katika ziara yake mkoani humo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akishindilia zege katika katika daraja dogo linalojengwa katika barabara ya lwilo mbongo na wanawake na vijana wa vikundi vya DARE na Ulonge wilayani Ludewa mkoani Njombe katika ziara yake mkoani humo.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
***************************
Na Mwandishi Wetu Ludewa Njombe
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amewtaka wanawake na vijana nchini kutumia changamoto zilizopo katika maneo yao kama fursa ya kujiajiri na kuajiri watu wengine.
Dkt. Ndugulile ameyasema hayo wilayani Ludewa mkoani Nombe wakati alipotembeela vikundi kazi vya wanawake na vijana vinavyojishughulisha na kutengeneza barabara na madaraja madogo wilayani humo.
Dkt.Ndugulile ameongeza kuwa vijana na wanawake wengi wamekuwa wakilalamika kukosa ajira hasa kwa walimaliza elimu ya juu ila wanawake na vijana wa wilaya ya Ludewa wamedhubutu kuchangamkia fursa ya kutengeneza barabara na madaraja madogo.
“Sijawahi kuona kitu kama hiki tangu nianze ziara zangu katika mikoa na wilaya hongereni mmedhubutu na mkaamua ktuia fursa hii kupatakujiajir ni mwanzo mzuri mtafika mbali” alisisitiza Dkt. Ndugulile.
Ameogeza kuwa jambo linalofanywa na vikundi hivyo linaendana moja kwa moja na dhana ya Maendeleo ya Jamii ya wananchi kushiriki katika shughuli za kimaendeleo katika maneo yao kwa kuamsha ari yao katika kushiriki shughuli hizo pamoja na kujiongezea kipato.
Aidha Dkt. Ndugulile amezitaka Hlmashauri nchini kuhimiza wanawake na vijana kujiunga katika vikundi vya kijasiriamali ili kuwawesha kupata mikopo ya kufanya biashara na miradi mbalimbali kama wanavyofanya wanawake na vijana wa wilaya ya Ludewa.
Dkt. Nduguile amewapa moyo wanawake na vijana hao wa wilaya ya Ludewa katika harakati za kutafuta kazi na kuwasihi vijana na wanawake wengine kutojibweteka wakisubiri ajira za kujiajiri bali wajiongeze na kujiajiri na hata kuajiri watu wengine.
“Jambo hili mnalofanya ni jambo jema la msingi litawasaidia kupata kipato na kujinua kiuchumi kwani kwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mhe.Rais Magufuli inasisitiza watu kufanya kazi hasa vijana na wanawake” alisema Dkt. Ndugulile
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kikundi cha DARE Bi. Theopista Mhagama amesema kuwa jumla ya vikundi 54 vimefanikiwa kujisajili katika Mamlaka mbalimbali ambazo zitawawezesha kuomba na kupata kazi za kutengeneza barabara na madaraja wilayani humo na Tanzania kwa ujumla
“Kwakweli tunafarijika sana kwani tumeamua kwa dhati kujikwamua kiuchumi na sio kukaa na kulalamika na kusbiri kufanyiwa kila kitu na Serikali wakati kama vijana na wanawake tunaweza kufanya kazi tukajiajiri na kuajiri wengine” alisema Bi. Theopista.
Ameongeza kuwa mpaka sasa wamepata kandarasi ya kujenga madaraja madogo katika barabara ya lwilo mbongo na yamefika katika asilimia 75 na wamedhutu kuomba tenda za ujenzi wa barabara na madaraja za kitaifa kwani wanakidhi vigezo kama wakandarasi wengine.