Aliyepo kushoto ni Mkurugenzi wa tamasha hilo,Dave Ojay katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa chuo hicho ,Ezra Mbogori na kulia kwake ni Mkurugenzi wa mipango wa chuo hicho,Sara Teri wakati wakizungumza na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya tamasha hilo la Kan Festival (Happy Lazaro)
…………….
Happy Lazaro,Arusha.
Zaidi ya wageni 5,000 kutoka nchi Saba ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki katika tamasha la sanaa na ufahamu (Kan Festival )litakalofanyika Januari 22 hadi 25 katika chuo cha maendeleo na ushirikiano wa kimataifa (MS -TCDC mkoani Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha,Mkugenzi wa tamasha hilo,Dave Ojay amesema kuwa,tamasha hilo linalenga kuwakutanisha watu mbalimbali likiwa na lengo kubadilishana uzoefu pamoja na kujifunza maswala mbalimbali yahusiyo maendeleo kwa faida ya nchi yetu.
Okay amesema kuwa,uwepo wa tamasha hilo utaleta mshikamano na umoja sambamba na kujitambua hasa katika maswala ya maendeleo ambapo litawalenga watu mbalimbali hususani Vijana wa vyuo vya elimu ya juu .
Amesema kuwa,kupitia tamasha hilo wataweza kuangalia maswala mbalimbali ya maendeleo yaliyofanywa na viongozi wa zamani na kuweza kuyaendeleza kwa pamoja na kuondokana na changamoto mbalimbali na kuhakikisha maswala tunayofanya yanaendana na wazee wa zamani.
Amesema kuwa,katika tamasha hilo watawashirikisha waonyeshaji mbalimbali wa Sanaa na tamaduni ambao wataweza kuwakilisha ujumbe wao kupitia Sanaa,tamaduni na muziki lengo likiwa ni kubadilishana mawazo na kuendeleza mahusiano.
Mkurugenzi Mkuu wa chuo hicho,Ezra Mbogori amesema kuwa,uwepo wa tamasha hilo utasaidia Sana kubadilishana mawazo baina ya wanafunzi hao wa vyuo na wageni kutoka nchi mbalimbali .
Alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi wa matabaka yote, wanafunzi ,Vijana kuhudhuria tamasha hilo maana watapata elimu ya vitendo na mambo mbalimbali katika kubadilishana ujuzi kutoka nchi zingine.
“Kiingilio katika tamasha hilo ni 15,000 kwa watu wazima na 5,000 kwa watoto huku watoto wenye umri chini ya miaka 12 wataingia bure ,hivyo nawaomba Sana mjitokeze kwa wingi katika tamasha hili kwani lina fursa za kutosha.”amesema.
Naye Mkurugenzi wa mipango wa chuo hicho, Sara Teri alitaja wanamuziki watakaoshiriki katika tamasha hilo kuwa Ni mwanamuziki kutoka nchini Tanzania ,Fid Q,Vitali Maembe ,Sandra Nankoma kutoka Uganda ,Juma Tutu kutoka Kenya ,Victor Kunonga kutoka Zimbabwe,Isabella Novela kutoka Mozambique .
Ametaja nchini zitakazoshiriki tamasha hilo kuwa ni pamoja na Kenya,Tanzania,Uganda, Mozambique,Burundi, Zimbabwe,Afrika Kusini na Congo.