Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Gelasius Byakanwa mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mtwara kwa ajili ya mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Newala Vijijini, Mhe. Rashid Ajali Akbar
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akipokelewa na Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Mtwara mara baada ya kuwasili nyumbani kwa aliyekuwa Mbunge wa Newala Vijijini, Mhe. Rashid Ajali Akbar kwa ajili ya mazishi yaliyofanyika leo nyumbani kwake Newala Mjini.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akisaini kitabu cha rambirambi ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Newala Vijijini, Mhe. Rashid Ajali Akbar nyumbani kwake Newala Mjini Mkoani Mtwara.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Newala Vijijini, Mhe. Rashid Ajali Akbar nyumbani kwake Newala Mjini Mkoani Mtwara.
Wananchi Mbalimbali wakiwa katika mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Newala Vijijini Mhe. Rashid Ajali Akbar yaliyofanyika leo nyumbani kwake Newala Mjini Mkoani Mtwara.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na viongozi wa serikali, wabunge na wananchi mbalimbali katika msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Newala Vijijini, Mhe. Rashid Ajali Akbar nyumbani kwake Newala Mjini Mkoani Mtwara.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)