TIMU ya KMC imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliofanyika jioni ya leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Ushindi huo unaifanya KMC ifikishe pointi 17 katika mchezo wa 17, ingawa inabaki nafasi ya 17 wakati Mtibwa Sugar inafikisha pointi zake 22 baada ya kucheza mechi 16 na inabaki nafas ya 10.
Katika mchezo wa leo, mabao ya KMC inayocheza Ligi Kuu kwa msimu wa pili mfululizo tangu ipande, yote yamefungwa Sadallah Lipangile dakika ya 18 akimalizia pasi ya Serge Tapei na la pili dakika ya 41 akimalizia pasi ya Ally Ramadhani.
Mtibwa Sugar inayofundishwa na kocha Zubery Katwila inapoteza mchezo huo wa Ligi Kuu ikitoka kufanya vyema kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kubeba taji hilo baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Simba kwenye fainali Jumatatu wiki hii Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Kikosi cha KMC Kilikuwa; Jonathan Nahimana, Ismail Gambo, Ally Ramadhani, Abdallah Mfuko, Jean Baptiste Mugiraneza, Kenny Ally, Hassan Kabunda/Kelvin Kijiri dk65, Emmanuel Mvuyekure, Sadallah Lipangle/Salim Aiyee dk85, Suleman Ndikumana na Serge Alian.
Mtibwa Sugar; Shaaban Kado, Kibwana Shomari, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Dickson Job, Cassian Ponera, Abdulhalim Humud, Awadh Salim/Haruna Chanongo dk46, Ally Makarani, Jaffary Kibaya, Onesmo Mayaya/Riphat Khamis dk52 na Salum Kihimbwa.