Home Mchanganyiko TANCDA YASISITIZA WAANDISHI KUANDIKA HABARI ZINAZOHUSU MAGONJWA YASIYOAMBUKIZWA

TANCDA YASISITIZA WAANDISHI KUANDIKA HABARI ZINAZOHUSU MAGONJWA YASIYOAMBUKIZWA

0

Meneja Mradi wa Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyoambukiza (TANCDA), Happy Nchimbi akizungumza na wanachama wa asasi ya (TOANCD) wakati akifungua mkutano wa mwaka wa Asasi hiyo ya Waandishi wa Habari ya Kuelimisha Jamii Kuhusu Magonjwa hayo kwenye ukumbi wa mikutano wa NIMR jijini Dar es salaam.

  Leon Bahati Mwenyekiti wa Asasi ya Kuelimisha Jamii kuhusu magonjwa yasiyoambukizwa inayoundwa na waandishi wa habari (TOANCD) akizungumza katika  mkutano huo kulia ni Exeperius Kachenje Makamu Mwenyekiti na Stella Nyemenohi Mhazini.

Exeperius Kachenje Makamu Mwenyekiti akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika taasisi ya utafiti ya NIMR jijini Dar es salaam.

Stella Nyemenohi Mhazini wa Asasi ya TOANCD akitoa taarifa ya fedha katika mkutano huo kulia ni Daniel Sembelya Katibu wa Asasi ya TOANCD na katikati ni Leon Bahati Mwenyekiti wa Asasi ya TOANCD.

Mmoja wa wajumbe wa mkutano huo akichangia hoja wakati wa majadiliano.

Mmoja wa washiriki wa mkutano huo ambaye ni machampioni wa kupambana na magonjwa yasiyoambukizwa akizungumza na kutoa ushuhuda katika mkutano huo.

baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mjadala na hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na washiriki.

Meneja Mradi wa Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyoambukiza (TANCDA), Happy Nchimbi Waandishi wa Habari nchini wameshauriwa kuandiaka habari zinazohusiana na magonjwa yasiyoambukiza ili kuipatia jamii elimu sahihi kuhusu magonjwa hayo

Happy Nchimbi ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa Asasi ya Waandishi wa Habari ya Kuelimisha Jamii Kuhusu Magonjwa hayo.

Alisema iwapo waandishi wa habari hasa wanaoandika habari za magonjwa yasiyoambukiza wataongeza juhudi kuandika habari hiyo jamii itaweza kuepuka magonjwa hayo.

Nchimbi alisema kwa siku za karibuni jamii imekuwa ikikabiliwa na magonjwa yasiyoambukiza hali ambayo inaonesha kuwa changamoto kubwa ni elimu na ufahamu wa namna ya kukabiliana na hali hiyo.

“Sisi TANCDA tunajitahidi kutoa elimu kuanzia ngazi ya shule lakini tuaamini iwapo tutashirikiana na waandishi wa habari elimu itafika kwa watu wengi na kwa haraka, hivyo tunawaomba tuungane katika hili kwani ni tatizo hasa mijini,” alisema.

Meneja Mradi huyo alisema hadi sasa wameweza kutoa elimu kwa watu zaidi ya 1,000 kutoka kwenye makundi mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa shule za sekondari.

Alisema shirikisho hilo litaendelea kutoa elimu katika makundi mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari ili wawe na uelewa kuhusu magonjwa yasiyoambukiza na kuyaandika kwa ufasaha.

Alisema magonjwa yasiyoambukiza yanatibika iwapo watu watafuata mtindo sahihi wa maisha ikiwemo kufanya mazoezi kila siku.

Mwenyekiti wa Asasi ya Waandishi wa Habari ya Kuelimisha Jamii Kuhusu Magonjwa Yasiyoambukiza, Leon Bahati alisema iwapo waandishi watajikita katika uandishi wa habari hizo jamii itaweza kubadilika na kujinusuru na magonjwa hayo.

Bahati alisema Watanzania wengi hawana uelewa kuhusu magonjwa hayo hivyo waandishi wakiandika kwa mfululizo habari hizo kutakuwa na mabadiliko.

“Tulikuwa tunafanya kazi hizi kwa mapenzi bila kuwa na usajili wa kudumu lakini kwa sasa tumepata usajili naombeni mtembee kifua mbele kwa kuandika habari za magonjwa yasiyoambukiza na mengine kwa kasi ya mwendokasi ili kunusuru jamii,” alisema.

Mwenyekiti huyo alisema mikakati ya asasi hiyo kwa kushirikiana na TANCDA ni kuhakikisha kazi za waandishi ambao wataandika habari hizo zinatambulika na kuheshimiwa ndani na nje ya nchi.

Katibu Mkuu wa Asasi hiyo, Daniel Semberya aliwataka wanachama kushirikiana na uongozi ili waweze kupata urahisi wa kupata taarifa kutoka kwa wataalam wa magonjwa yasiyoambukiza.

Semberya aliwaomba waandishi wa habari kujiunga na asasi hiyo ili kuwepo na mtandao mpana wa kuandika habari za magonjwa yasiyoambukiza.