********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Simba leo imeibamiza timu ya Mbao Fc mabao 2:1 katika Uwanja wa Ccm Kirumba na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi Kuu.
Simba ilicheza kwa presha kubwa ikihitaji goli la mapema kwani walikuwa wanalisakama lango la mpizani mpaka kuwachukua dakika 41 bao la kuongoza kwa kipindi cha kwanza lililofungwa na winga Hassan Dilunga.
Kipindi cha pili Simba ilirudi kwa kasi hivyo dakika ya 46 ilifanikiwa kupata bao la pili lililofungwa na kiungo wa klabu hiyo Jonas Mkude.
Mbao Fc ilipata bao la kufutia machozi dakika ya 52 kupitia kwa Waziri Jr.
Simba sasa inajiandaa kuwakabili timu ya Alliance siku ya Jumapili katika uwanjka huohuo wa Ccm Kirumba.