Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndejembi akizungumza na wenyeviti na watendaji wa vijiji vyote vya Wilaya hiyo katika mkutano wa pamoja alioutisha wenye lengo la kujadili maendeleo ya Wilaya hiyo.
Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Kongwa, Job Ndugai akizungumza na wenyeviti na watendaji wa vijiji katika mkutano wa pamoja uliotishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Deo Ndejembi.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Dwo Ndejembi (kushoto) akiteta jambo na Spika wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kongwa, Job Ndugai kwenye mkutano wa pamoja na wenyeviti na watendaji wa vijiji ndani ya Wilaya hiyo.
Wenyeviti na Watendaji kutoka vijiji 87 vya Wilaya ya Kongwa wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo (hayupo pichani) walipokutana kwa mara ya kwanza tangu wenyeviti wachaguliwe kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 24 mwaka jana.
………………
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Deo Ndejembi amekutana na Wenyeviti na Watendaji wa Vijiji vyote vya Wilaya hiyo na kuagiza kila mmoja anasimamia maendeleo ya elimu ndani ya eneo lake kwa kuhakikisha kila mwanafunzi aliechaguliwa kuingia kidato cha kwanza anaripoti shuleni na mzazi atakaemkwamisha mtoto atachukuliwa hatua kali za kisheria.
” Kongwa hatutaki mchezo na elimu, wakati ambapo serikali inapambana kuifanya Nchi yetu kufikia Uchumi wa kati ni lazima pia sisi tunaomsaidia kazi Rais Magufuli tuhakikishe tunakuza sekta ya elimu ili kuzalisha kundi kubwa la wasomi ambalo litakua msaada kwa Taifa. Hatutoruhusu kuona mzazi yeyote anashindwa kumpeleka shule mtoto ambaye amechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza,” DC Ndejembi.
Kwa upande wake Spika wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kongwa, Mhe Job Ndugai amewataka wenyeviti hao kuwaongoza wananchi wao kwa haki bila upendeleo wal kupokea rushwa na kuwataka kuwa na moyo wa kizalendo kama alionao Rais Magufuli huku akiwasisitizia kuhakikisha wanasimamia maendeleo ya elimu ndani ya Kongwa.
Akitoa tathimini ya ufaulu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kongwa, Dk Omary Nkuru amesema kiwango cha ufaulu kwa matokeo ya kidato cha nne ndani ya Wilaya hiyo yameongezeka ambapo imekua ya pili kimkoa nyuma ya Jiji la Dodoma huku idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano ikiwa ni 670 kulinganisha na mwaka jana ambapo walikua 300